Na Julieth Mkireri, MAIPAC Rufiji
Wafugaji Wilayani Rufiji wameishukuru Serikali ya Wilaya kwa kushirikiana na Chama cha Wafugaji kwa kujenga maeneo kwa ajili ya Wafugaji kupitia mpango wa matumizi bora ya ardhi, na kupatiwa hati miliki.
Zaidi ya Wafugaji 50 wamepatiwa hatimiliki hizo hali itakayopunguza migogoro ya mara kwa mara kati ya Wafugaji na Watumiaji wengine wa ardhi.
Ugawaji wa hati miliki hizo umefanywa na Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Mwang'onda Jana Aprili 26, 2026 katika kata ya Chumbi baada ya Mwenge kutembelea eneo maalumu kwa ajili y'all wafugaji.
Pongezi za Wafugaji hao zimetolewa na Lisesi Tunung'u ambaye alisema awali maisha yao yalikuwa ya kuhama hama na kwasasa wanamiliki ardhi yao kuendesha shughuli za ufugaji nimepata ardhi.
Kwa upande wake Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa Wazo Mwang'onda ameipongeza Halmashauri ya Mji Rufiji kwa kutekeleza mpango wa Ranchi ndogo na kupunguza migogoro,.
"Nawapongeza Wilaya ya Rufiji kwa kazi hii nzuri na wawekezaji wetu ambao wamewekeza katika Ufugaji kwasababu hii ni biashara, Mwenge wa Uhuru umeridhishwa na utekelezaji wa Ranchi hizi." amesema Mwang'onda.
Awali akisoma taarifa ya utekelezaji wa Ranchi hizo Mkuu wa Divisheni ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi Halmashauri ya Mji Rufiji Ryoba Magabe alisema Wilaya ya Rufiji inatekeleza mpango wa Ranchi ndogo kwa ajili ya kuwapanga Wafugaji.
Amesema wafugaji watapangwa kwenye vitalu Maalumu vya Ufugaji lenye ukubwa wa hekari 125, ambapo kwa Kata ya Chumbi kuna vitalu 58.
Mwenge wa Uhuru umekagua na kuweka jiwe la Msingi miradi 7 yenye thamani ya Shilingi Bilioni 4.95.

No comments:
Post a Comment