ALLYS TAILOR: VIJANA TUMIENI FURSA YA UJIO WA AFCON ARUSHA KUJIKWAMUA KIUCHUMI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 2 May 2026

ALLYS TAILOR: VIJANA TUMIENI FURSA YA UJIO WA AFCON ARUSHA KUJIKWAMUA KIUCHUMI

 


Na Mwandishi Wetu maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


 Vijana Nchini wametakiwa kutumia fursa ya ujio wa michuano ya Afcon kama fursa ya kujiinua katika kipato.


Wametakiwa wasiishie kuwa mashabiki wa soka pekee wakati wa michuano hiyo na badala  waigeuze michuano hiyo kuwa fursa ya kujipatia kipato.


Wito huo umetolewa na Mbunifu na Fundi maarufu wa mavazi jijini Arusha ambaye pia ni Mkurugenzi wa ALLY'S TAILOR, Ndugu Ally Madongo, wakati akizungumza na Maipac Media.


Ally ambaye amekuwa katika tasnia hiyo ya ubunifu wa mavazi na ufundi kwa zaidi ya miaka kumi Sasa, amesema ujio wa Afcon katika jiji la Arusha ni bonge la fursa na hivyo vijana wenzake waichangamkie.


Amesema kwasasa yeye na wataalamu wake wa mavazi wanaumiza vichwa  na vazi ambalo litakuwa alama kwa vijana mashabiki wa soka Arusha wakati wa Afcon.


"Natamani kama Mbunifu kijana wa mavazi niibuke na vazi moja maridadi lenye changanyiko wa rangi za bendera yetu ya taifa ambalo linaweza kuwa la mtoko wakati wa game za Afcon",alisema Bwana Ally Madongo.


Madongo ambaye anatoka katika familia maarufu  ya mafundi na wabunifu wa mavazi ya Madongo, amesema kwasasa anaendelea pia na program maalum ya kuwasaidia vijana wanochipukia katika fani ya ufundi na ubunifu wa mavazi ili wafikie au hata kupita hatua aliyofikia yeye.


Ally's Tailor waliopo Makao Mapya jirani na Ofisi za CCM kata ya Levolosi jijini  Arusha, kwasasa wanaendelea kutoa huduma ya mavazi ya kila aina kwa wanaume na Wanawake.


Baadhi ya mavazi hayo ni Suti za Wanaume na Wanawake, Kaunda Suti, sare za shule na za makampuni mbalimbali pamoja na mavazi ya asili.


Wanapatikana katika mitandao ya kijamii kwa jina la @ally'stailor na kwenye namba ya simu 0686616369.


Ally's Tailor wamekuwa chaguo la watu wa Rika zote!

No comments: