Chama Cha Mawakala Wa Mabasi Mkoa wa Arusha (CMMA), Chapongezwa na Viongozi wa Dini - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 2 May 2026

Chama Cha Mawakala Wa Mabasi Mkoa wa Arusha (CMMA), Chapongezwa na Viongozi wa Dini




Na Kassim Kiko,Maipac Arusha


maipacarusha20@gmail.com 


Chama Cha Mawakala Wa Mabasi Mkoa wa Arusha (CMMA),Kimepongezwa kwa kuwa mdau mkubwa wa Amani na Maadili katika Jamii.


Aidha CMMA imepongezwa kwa kuipa hadhi kazi ya Mawakala wa Mabasi mkoani Arusha na kuondoa dhana iliyokwepo kwa muda mrefu kuwa wanaofanya kazi Stand ni wababe na wahuni.


Pongezi hizo zimetolewa kwa nyakati tofauti na Viongozi wa Dini wakati wakitoa mada katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa CMMA uliofanyika katika hoteli ya Golden Rose jijini Arusha.


Mhadhiri wa Kimataifa na Naibu Mkuu wa Chuo Cha Ahlul Bayti ABC Cha jijini Arusha Sheikh Dr Abdulrazaq Ameir Juma, amesema kwa jinsi alivyoifahamu stand ya mabasi ya Arusha kwa miaka iliyopita ni wazi kwamba uwepo wa CMMA umeibadilisha hadhi ya stand yenyewe na kukuza heshma ya wanaofanya kazi Mahali hapo.


"Mimi ni mzaliwa wa hapa mjini Arusha na najua sekeseke zote zikizokuwa zikifanyika katika kituo kikuu Cha Mabasi,Kwa uwepo wa CMMA kumeleta taswira nzuri kuwa hapa ni eneo la kazi ni sio genge la wahuni!",alisema Dr Abdulrazaq ambaye pia ni mtaalam wa Elimu ya Maendeleo ya Jamii.


Kwa upande wake Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Maridhiano na Amani Tzania ambaye pia ni Balozi wa Amani DUNIANI, Askofu Dr Israel Maasa Ole Gabriel amesema kabla ya aujio wa CMMA ilikuwa unapofika kituo cha Mabasi unagombewa na wahuni kama mpira wa kona.


Askofu Maasa amewasifu CMMA kwa kuhuburi Amani na UMOJA wakitaifa wanapokuwa katika shughuli zao za kila siku.


Awali akiwasilisha taarifa ya Chama hicho Mkiti wa CMMA Ndugu James Benard alisema wachama wa CMMA wamedhamiria kujikwamua kiuchumi kupitia Chama hicho na wataendelea kushirikiana na serikali katika kuhuburi Amani na Maendeleo.


James amempongeza serikali ya awamu ya sita Kwa juhudi zake za kuboresha miundombinu ikiwemo ujenzi wa kituo cha kisasa cha mabasi katika eneo la Bondeni City jijini Arusha.


Ameiomba serikali kuwafikiria CMMA kama Wadau muhimu katika sekta ya usafirishaji wa abiria mkoani Arusha nao wapate maeneo ya kufanyia shughuli zao katika stendi hiyo mpya ya kisasa.


Kwa Upande wake Naibu Katibu Mkuu wa CMMA Bwana Shwaibu Sachu, amesema mahusiano yao na taasisi za Dini na zile za kimaendeleo ikiwemo bank ya CRDB kumewapa wigo mpana wanachama kujichanganya na Jamii na kujua mambo yanavyoendelea nje ya eneo lao la kazi.


Akitoa neno la shukrani Makamu Mkiti wa CMMA Ndugu Maulid Nyekanyeka 'Gado', amesema maboresha yaliyotokea katika Mkutano Mkuu wa mwaka huu ya kuwaalika watoa mada mbalimbali yanalenga kuwapa wigo mpana wa ufahamu wa mambo wanachama wao.


Naye Mkiti wa Baraza la Wazee wa CMMA Bwana Hussein Bwengo, amesema Baraza limekuwa na jukumu la kutoa busara na kuleta uwiano mzuri baina ya Wazee na vijana ambao ndio wengi zaidi katika shughuli za kila siku katika kituo kikuu cha mabasi cha Arusha.

No comments: