Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ametaka utu, heshima na haki za wafungwa hususan wanawake ziheshimiwe, kwa kuwa wana mahitaji ya ziada na maumbile tofauti na wanaume.
Dkt Samia ametoa kauli hiyo leo, Jumamosi Mei 9, 2026 wakati wa hafla ya kuhitimisha mafunzo ya uongozi ngazi ya juu Kodi namba 48 kwa mwaka 2025/26 katika Chuo cha Taaluma ya Urekebishaji Tanzania.
"Kwa hiyo wale mnaochunga wafungwa wanawake, haki na utu wao naomba uheshimiwe. Ni wahalifu wamekosa wameadhibiwa, lakini utu wao naomba uheshimiwe," amesema.
Ametaka wafungwa hao, wapate nafasi yao kama wanawake kwa kuwa maumbile yao ni tofauti na wanaume.


No comments:
Post a Comment