Na Mwandishi wetu, Karatu
maipacarusha20@gmail.com
Halmahauri ya Karatu,Arusha kwa kushirikiana na wataalamu wa ardhi wa wilaya hiyo wanatarajia kuisha mji huo uweze kukaa katika mpangilio mzuri wa kitalii
Uishaji huo utaendana na fursa mbalimbali ambazo zinapatikana zaidi katika wilaya hiyo Hali ambayo itachangia kwa kiwango kikubwa ongezeko la wawekezaji ndani ya wilaya hiyo
Hayo yalielezwa wiki iliopita na Bw Faraji Rushagama ambaye ni Afisa Ardhi pamoja na mwangalizi wa ofisi za ardhi wilaya ya karatu wakati aliongeza kwenye Baraza la madiwani kutoka katika kata mbalimbali za halmahauri hiyo
Bw Faraji alisema kuwa Karatu ni mji ambao unakuwa kwa kiwango Cha Kasi sana sasa ndio maana wameamua kuweka mikakati maalumu wa kuhakikisha kuwa wanabadilisha hata muobekano wa mji huo
Aliongeza kuwa uishaji huo utaanzia kwa kuangalia vigezo kama uwanja wa ndege wa manyara ambapo uishaji utaenda mpaka maeneo ya ngorongoro
"Karatu pamoja na wizara kwa pamoja tumejidhatiti kuhakikisha kuwa Karatu unavutia Tena kwa kiwango kikubwa sana hivyo fursa za uwekezaji nazo zinatarajiwa kuongezeka kwa Kasi kubwa sana"aliongeza
Wakati huo huo alisema kuwa kwa mji huo wa kitalii unaonekana kukuta kwa kiasi kikubwa sana tayari ofisi yake imeshaanza kuangalia mashamba mawili makubwa sana ambayi yatagawiwa kwa wananchi wa karatu
Alisema,kuwa uwepo wa mashamba hayo utaweza kusaidia kupunguza ujenzi holela lakini pia wimbi kubwa la migogoro ya ardhi.
"Karatu Bado tuna wimbi kubwa la migogoro ya ardhi pamoja na ujenzi holela lakini tunaamini kupitia uwepo wa mashamba haya mawili makubwa hivi vitu havitakuwepo kabisa Mimi nipo kuhakikisha kuwa Karatu inakuwa na mabadiliko makubwa sana kwenye sekta ya Ardhi,nataka watu waje hapa wajifunze"aliongeza
Alihitimisha kwa kusema kuwa nao wananchi ambao Wana miliki ardhi wanatakiwa kujua na kutambua kuwa wanapaswa kulipa Kodi ya Pango la ardhi kila mwaka kama vile Sheria inavyowataka kulipa na kutolipa kodi hiyo kunaweza kusababisha kujikosesha sifa.
Kwa upande wa madiwani wa Baraza Hilo walisema kuwa kupitia mikakati ambayo wamesomewa na kuiona katika Ofisi hiyo wanatarajia Karatu kuwa mji wa mfano Duniani kote
Madiwani hao walisema kuwa Mpangalio mzuri wa mji utaweza kuwavutia wawekezaji wengi kuja Karatu lakini hata Watalii kutoka maeneo mbalimbali duniani Kuna katika eneo Hilo la Karatu.
Naye mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Karatu na Diwani wa Kata ya Mbulumbulu, Mhe. Engliberth Qorro, alisema na kusisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya madiwani na wataalamu wa halmashauri ili kuhakikisha miradi ya maendeleo inatekelezwa kwa ufanisi na kuleta matokeo chanya kwa wananchi wa Wilaya ya Karatu.
Kikao hicho ni sehemu ya vikao vya kisheria vya halmashauri hiyo ambavyo vinavyofanyika ili kuhakikisha usimamizi mzuri wa rasilimali za halmashauri na kuimarisha maendeleo ya wananchi.
Mwisho

No comments:
Post a Comment