Profesa Kabudi: Yaliyotokea Oktoba 29 sio ya kawaida, hayafanani na nchi yetu - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 16 May 2026

Profesa Kabudi: Yaliyotokea Oktoba 29 sio ya kawaida, hayafanani na nchi yetu

 


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Uratibu na Wenye Ulemavu, Profesa Palamagamba Kabudi, amesema yaliyotokea Oktoba 29, 2025 hayakuwa mambo ya kawaida na hayafanani na Taifa la Tanzania.


Kwa sababu ya uhalisia huo, Profesa Kabudi, amesema ni vema kama Taifa kukubaliana kwamba yasitokee tena ‘Never Again’ kauli ambayo imetumika na mataifa mbalimbali yalipokumbwa na mambo yasiyo ya kawaida.


Profesa Kabudi, ameeleza hayo jijini Dar es Salaam leo, Mei 16, 2026 alipozungumza katika moja ya majopo wakati wa Kongamano la Vijana lililobeba ujumbe wa ‘Never Again’ inayomaanisha yasitokee tena


“Zipo nchi, zilikumbwa na misukosuko, tufani na baadaye zikasema never again what happened yesterday. Mmechukua kaulimbiu inayoashiria kwamba kuna lililotokea si la kawaida, halifanani na nchi yetu na limetutikisa,” amesema.


Aidha, Profesa Kabudi amesema chini ya uongozi wa Rais Dkt Samia Suluhu Hassan, ndipo mipango mingi iliyopangwa na Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Nyerere, imetekelezwa ikiwemo ujenzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JHPP).

No comments: