Wakili Marathon kufanyika uwanja wa Jamuhuri Dodoma May 31 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 25 May 2026

Wakili Marathon kufanyika uwanja wa Jamuhuri Dodoma May 31

 



Na Queen Lema,Dodoma


maipacarusha20@gmail.com 


Chama Cha Mawakili wa Serikali kwa kushirikiana na wadau wengine wameandaa mbio (wakili marathon) ambapo mbio hizo zitafanyika May 31 Dodoma


Akizungumza na vyombo vya habari mapema Jana Katibu wa chama hicho Wakili Rashid Mohamed alisema kuwa mbio hizo zitawajumuisha wadau mbalimbali 


Wakili Rashid alisema kuwa lengo halisi la mbio hizo ni kuwajumuisha wadau mbalimbali wakiwemo wananchi na waweze kuona kuwa mawakili ni  marafiki wa jamii.


"Hizi mbio zitawajumuisha watu wengi na ninapenda kuwaalika wanaopenda kukimbia waweze kujumuika na sisi kwani riadha ni sehemu ya mazoezi kwenye mwili"aliongeza.


aliendelea kwa kudai kuwa wakili marathon pia itakuwa na mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na utoaji wa zawadi kwa watakoweza kukimbia na kushinda.


Alidai kuwa katika mbio hizo ambazo ni Half Marathon wataweza kukimbia kwa umbali wa kilomit 21,10 pamoja na kilomita 5


"Gharama za kukimbia katika mbio hizi ni ndogo sana ambapo kiasi kinachoitajika ni sh elfu 40 pekee na atakayeweza kukamilisha Hilo atapewa Medani tuwaombe jamii bila kuchagua rika,Wala Tasnia yoyote ile waje wajumuike na sisi"aliongeza 


Alihitimisha kwa kusema kuwa mbio hizo zitafanyika Katika uwanja wa Dodoma May 31 na kuhudhuriwa na viongozi wengi wa Heshima


Mwisho

No comments: