EAC YATAKIWA KUIMARISHA SHERIA ZA KULINDA WATUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 26 June 2026

EAC YATAKIWA KUIMARISHA SHERIA ZA KULINDA WATUMIAJI WA MITANDAO YA KIJAMII

 



NA Mwandishi wetu  ARUSHA


maipacarusha20@gmail.com 


Wito umetolewa kwa serikali za nchi za Afrika Mashariki kuharakisha uundaji wa sheria na sera madhubuti za kulinda watumiaji wa mitandao ya kijamii dhidi ya unyanyasaji wa kidijitali, huku wanawake na watoto wa kike wakitajwa kuwa miongoni mwa waathirika wakuu wa matumizi mabaya ya teknolojia.




Akizungumza katika kilele cha Kongamano la Pili la Mazungumzo ya Kizazi kwa Kizazi la Wanawake wa Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC), Mwenyekiti wa Jukwaa la Wanawake la Jumuiya hiyo, Fatuma Ndangiza, amesema matumizi mabaya ya mitandao ya kijamii yameongeza vitendo vya udhalilishaji na ukatili wa kijinsia, hivyo akazitaka serikali na mabunge kuimarisha mifumo ya kisheria ya kulinda watumiaji wa majukwaa ya kidijitali.


Naye  Mwenyekiti wa jukwaa la wanawake JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI Fatuma Ndangiza


Aidha, Ndangiza amesisitiza umuhimu wa kuongeza uwekezaji katika elimu ya usalama wa kidijitali, hasa kwa wanawake na wasichana, ili kuwajengea uwezo wa kutambua na kukabiliana na vitendo vya unyanyasaji mtandaoni. Amesema pamoja na kuwepo kwa sheria, elimu na uelewa wa matumizi salama ya teknolojia ni nguzo muhimu katika kujenga mazingira salama ya kidijitali kwa wananchi wote


Kwa upande wake, Mbunge wa Bunge la Afrika Mashariki (EALA), Dkt. Gladness Salema, aamewataka vijana kutumia mitandao ya kijamii kwa uwajibikaji na kuzingatia maadili ya matumizi ya teknolojia. Amesema majukwaa ya kidijitali yanapaswa kutumiwa kujifunza, kukuza ubunifu, kuanzisha biashara, kupata ajira na kushiriki katika maendeleo ya jamii, badala ya kusambaza taarifa potofu, lugha za chuki au vitendo vinavyochochea, Huku mmoja wawashuriki akieleza umuhimu wa jukwaa hilo

No comments: