TCL Yatua Arusha, Yatangaza Punguzo la Asilimia 23 - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 26 June 2026

TCL Yatua Arusha, Yatangaza Punguzo la Asilimia 23

 





Na Mwandishi wetu,Arusha


maipacarusha20@gmail.com 


Wakazi wa Jiji la Arusha wamepata fursa ya kununua vifaa vya kisasa vya umeme kwa bei nafuu kufuatia kampuni ya TCL kufungua rasmi duka lake jipya huku watanzania wakipewa elimu ya matumizi sahihi ya vifaa vya umeme ili kuepusha madhara ya uharibifu yanayotokana na matumizi yasiyiyo sahihi.



 Katika uzinduzi huo uliofanyika Arusha na kuhudhuriwa na maelfu ya wakazi wa Arusha Meneja wa duka hilo, Faisal Salum, amesema kampuni imeanza kwa kutoa punguzo la asilimia 23 kwa bidhaa mbalimbali, ambapo ofa hiyo itadumu kwa mwezi mzima.


Salum amesema kufunguliwa kwa duka hilo kutachangia kuongeza ajira kwa vijana wa Kitanzania, sambamba na kutoa elimu kwa wateja kuhusu matumizi sahihi na salama ya vifaa vya umeme ili kuongeza ufanisi na kudumu kwa bidhaa hizo.


Aidha, ameeleza kuwa TCL ni chapa inayotambulika kimataifa na imejijengea sifa kubwa katika sekta ya vifaa vya kielektroniki, akiwahimiza Watanzania kutumia fursa ya punguzo hilo kwa kutembelea duka hilo na kujionea bidhaa mbalimbali zenye ubora wa hali ya juu.


Salum ametoa wito kwa wakazi wa Arusha na Watanzania kwa ujumla kufika dukani hapo mapema ili kunufaika na ofa hiyo maalumu kabla ya kumalizika.


Alihitimisha kwa kusema kuwa watanzania wanatakiwa pia kukimbilia dukani hapo ili kuweza kupata elimu ya matumizi ya vitu mbalimbali  vya umeme 


Mwisho

No comments: