Rais Samia Suluhu Hassan, amesema pamoja na kuyapongeza mashirika yanapofanya vizuri, hatavumilia uzembe na matumizi mabaya ya fedha za umma atakapobaini.
Rais Samia ameyasema hayo leo, Jumanne Juni 30, 2026 alipohutubia hafla ya Siku ya Gawio iliyofanyika Ikulu, jijini Dar es Salaam.
“Tutajipongeza tunapofanya vizuri, vilevile tutajirekebisha au kujiimarisha pale penye mapungufu. Hatutasita kuchukua hatua pale tutakapobaini uzembe na matumizi mabaya ya fedha za umma, na ndio maana nasisitiza tathmini,” amesema.

No comments:
Post a Comment