KIHONGOSI KUTIKISA WLAYA TATU ZA ARUSHA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 1 June 2026

KIHONGOSI KUTIKISA WLAYA TATU ZA ARUSHA

 



Na Mwandishi wetu,Arusha


maipacarusha20@gmail.com 


Chama Cha mapinduzi  mkoa wa Arusha kinatarajia kumpokea Katibu wa itikadi uenezi na  Mafunzo,Kenani Kihongosi ambapo atafanya ziara  kwenye wilaya tatu za mkoa wa Arusha kuanzia June 4


Akizungumza na waandishi wa habari mapema Leo Katibu wa  Siasa na uenezi mkoa wa Arusha ,Bw Saipulani Ramsey Alisema kuwa watampokea kiongozi huyo ambaye atakuwa Arusha kwa muda wa siku 3 


Alisema kuwa Kenani anafanya ziara zake kote nchini ikiwa ni mkakati maalumu wa  Ccm baada ya kukamilika kwa uchaguzi mkuu.


Alifafanua kuwa Kenani  ataanzia ziara yake June nne katika wilaya ya Karatu,June 5 atakuwa Arumeru,na siku ya June 6 atakuwa Arusha mjini


"Lengo la kuzunguka kw a kiongozi huyo ni kukutana na wananchi lakini pia kukagua miradi mbalimbali ambayo inatekelezwa na Serikali"aliongeza 


Katika hatua nyingine alisema kuwa wananchi wanatakiwa kujitokeza kwa wingi sana lakini pia hata kutoa madukuduku yao ambayo wanayo


"Kwenye hizi wilaya ambazo zitakuwa na ugeni huu wa Kitaifa tunawasihi sana wananchi waje kusikiliza hoja za Ccm ,walete yale ambayo yanawakwamisha au yameshindwa kutekelezwa ipasavyo,na miradi inayotekelezwa na niya wananchi hivyo wajitokeze"aliongeza 


Akiongelea utendaji kazi wa Ccm mkoa wa Arusha alisema kuwa mkoa umeweza kufanya ziara katika kata 101 katu ya kata 161


"Baada ya uchaguzi mkuu huwa tunafanya tathimini kwa wananchi wetu,na tumeshamaliza kata hizo zilizobaki Bado tutahakikisha kuwa tunazifikia ikiwa ni pamoja na kuangalia changamoto zilizopo ndani ya kata hizo"aliongeza.


Alihitimisha kwa kusema kuwa kwa kipindi kilichopita Cha uchaguzi mkuu Ccm ilifanikiwa kushinda kwa asilimia zaidi ya 98 na kwa  uchaguzi ujao wa mwaka 2030 wanatarajia kufikia asilimia 100.

No comments: