Mahakama ya Afrika Imeiamuru Tanzania Kufuta Adhabu ya Kifo na Mfumo wa Unyongaji! - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 7 June 2026

Mahakama ya Afrika Imeiamuru Tanzania Kufuta Adhabu ya Kifo na Mfumo wa Unyongaji!



 




Mwandishi Wetu Maipac 

maipacarusha20@gmail.com 


Mahakama ya Afrika ya Haki za Binadamu na Watu (AfCHPR) iliyopo jijini Arusha, imetoa uamuzi mkubwa unaoitaka Serikali ya Tanzania kuondoa haraka vifungu vyote vya sheria vinavyolazimisha adhabu ya kifo pamoja na njia ya kunyonga, ikitaja taratibu hizo kuwa zinakiuka haki ya kuishi na utu wa binadamu.




Uamuzi huo umefuatia kesi iliyofunguliwa na wafungwa watatu wa Gereza Kuu la Butimba mkoani Mwanza—Chacha Jeremiah, Methew Jeremiah Daud, na Paschal Ligoye Mashiku—waliokuwa wamehukumiwa kunyongwa hadi kufa kwa kosa la mauaji.

Mambo makubwa yaliyojiri kwenye hukumu hiyo:


Uhuru wa Majaji: Mahakama imesema adhabu ya kifo ya lazima inamnyima jaji uwezo wa kutumia busara zake kuzingatia mazingira ya kosa na mtuhumiwa kabla ya kutoa adhabu.




Agizo kwa Serikali: Tanzania imeamriwa kufuta adhabu hizo, kuwaondoa waombaji kwenye safu ya kifo (death row), na kuwepo kwa utaratibu wa kesi zao kusikilizwa upya upande wa adhabu pekee.




Fidia: Mahakama imeamuru kila mwombaji alipwe Shilingi laki moja (TZS 100,000) kama fidia ya madhara ya kisaikolojia na kiadili waliyopata.



Uamuzi wa Majaji: Hukumu hiyo imesomwa Juni 5,2026 na jopo la majaji 8 wakiongozwa na Rais wa Mahakama hiyo, Jaji Blaise Tchikaya. Hata hivyo, baadhi ya majaji kama Jaji Rafaâ Ben Achour na Jaji Modibo Sacko walikuwa na maoni tofauti (dissenting opinions) kuhusu muda wa upelelezi na kiasi cha fidia.



Serikali imepewa miezi mitatu kuchapisha hukumu hii kwenye tovuti za Idara ya Mahakama na Wizara ya Katiba na Sheria.

No comments: