MAIPAC, MISA Tan, Media Brain wataka ushirikishwaji zaidi Vyombo vya habari kutetea Maslahi ya Umma - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 25 June 2026

MAIPAC, MISA Tan, Media Brain wataka ushirikishwaji zaidi Vyombo vya habari kutetea Maslahi ya Umma

 




Mwandishi wetu,Dodoma


maipacarusha20@gmail.com 


Taasisi ya Wanahabari ya kusaidia jamii za pembezoni (MAIPAC) na Taasisi ya Habari Kusini mwa Afrika tawi la Tanzania (MISA-Tan) na Media Brain wametaka kuongezwa ushirikishwaji wa vyombo vya habari katika kuandika na kutangaza zenye maslahi kwa umma.


Wakizungumza katika mjadala juu ya ushirikishwaji wa vyombo vya habari na Utetezi wa Kidijitari Tanzania June 24,2026 jijini Dodoma, Mkurugenzi wa MAIPAC ,Mussa Juma na Mwenyekiti wa MISA Edwin Soko na Nelvin Meena kutoka taasisi ya Media Brain  wamesema bado vyombo vya habari havishirikishwi ipasavyo ili kuongeza uelewa katika jamii.



Juma amesema, Vyama vya Mawakili na Azaki  ambazo zinafanya utetezi wa haki za binaadamu, zinapaswa kutumia zaidi vyombo vya habari vya asili na kidigitari ili jamii kuelewa na kushirikishi katika masuala ya utetezi wa haki za binaadamu.


Juma amesema, Tafiti iliyofanywa na taasisi ya Twaweza imebaini bado jamii inategemea vyombo vya habari kupata taarifa sahihi na asilimi 87  wanategemea Radio kupata taarifa.

Mkurugenzi wa MAIPAC Mussa Juma 


"Tuna Radio 260 ambazo zimesajiliwa nchini kote hivyo kuna fursa ya kuzitumia ,lakini pia Mtandao wa Intenet unawafikia karibu watanzania 56.3 na kuna laini za simu 99.3 millioni ambazo zinatumika hivyo kuna fursa za kidigitari kufanya utetezi"amesema


Soko amesema, licha ya wananchi kupunguza imani kwa taarifa za vyombo vya habari vya asili hasa kutokana na vikwazo lakini bado kuna wananchi wanavitegemea kupata taarifa sahihi.


"Kwa upande wa taarifa za kidigitari MISA Tan  tunakusudia kuogeza jitihada za kuwajengea uwezo wanahabari zaidi ya 200 katika kuandika habari sahihi zenye maslahi kwa umma "amesema


Kwa upande wake Meena, amesema ni muhimu wanahabari kujengewa uwezo wa kufanya kuandika habari za kina juu ya masuala ya utetezi wa haki za binaadamu .


"Sio kila mwandishi anaweza kuandika na kutangaza vyema mambo ya haki za binaadamu hivyo suala la kuwajengea uwezo na kuwashirikisha zaidi haliepukiki"alisema


Akiongoza mjadala huo, Mtaalam wa masuala ya Azaki, Annastazia Rugaba amesema ni muhimu suala la uhuru wa vyombo vya habari kutazamwa  hasa kipindi hikiya utekelezwaji wa Dira ya taifa ya Maendeleo ya 2050.


Mkutano  huo wa Wadau na kuhusu Mikakati ya Utetezi wa Utawala wa Sheria, Nafasi ya Kiraia na Marekebisho ya Sheria Nchini Tanzania umeandaliwa  mashirika manne.


Mashirika hayo ni Mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu (THRDC), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) chama cha mawakili Afrika ya Mashariki, Chama cha Mawakili Zanzibar (ZAFELA) na Chama cha  Mawakili wa Pan Afrika (PALU) chini ya mradi wa Kulinda Utawala wa Sheria, Nafasi ya Kiraia na Uwajibikaji Tanzania kupitia Ushirikiano na Ubia Ulioboreshwa ( SCATZ) na unafadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya.


Mwisho

No comments: