Sioni dhamira ya dhati kupata Katiba Mpya-Kibamba - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 25 June 2026

Sioni dhamira ya dhati kupata Katiba Mpya-Kibamba

 

Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa nchini, Deus Kibamba


Wakili Paul Kisabo wa THRDC


Mwandishi wetu,Dodoma


maipacarusha20@gmail.com 



Mchambuzi wa Masuala ya Kisiasa nchini, Deus Kibamba amesema haoni dhamira ya dhati Kwa viongozi wa Serikali kuwapatia watanzania kwa wakati Katiba Mpya.


Akizungumza katika Mjadala juu ya fursa zilizopo kimataifa na Kikanda katika  nafasi za Kiraia na Ulinzi wa Haki za Binadamu, Kibamba amesema katika siku za karibuni kumeanza kutolewa kauli za kufanyika  maboresho ya Katiba badala ya kuandikiwa upya Katiba ya Nchi.


"Binafsi ukiniuliza suala la kupata Katiba mpya ambayo ndio msingi wa changamoto nyingi kwenye jamii sioni dhamira ya dhati ya viongozi na hivyo Asasi za kiraia na wananchi lazima tuungane  kupata Katiba Mpya"amesema 


Awali, wakizungumza katika Mjadala huo,Wakili Jebra Kambole,Wakili PraiseGod Joseph na James Marenga walisema bado kuna fursa kushirikiana na vyombo vya kimataifa na Kikanda kutatua changamoto zilizopo nchini.


Wakili Jebra Kambole hata hivyo amesema kesi za maslahi ya Umma ambazo zimefunguliwa na baadhi kushinda zimekuwa na manufaa makubwa ikiwepo kuanza kurejesha uwajibikaji na utawala wa Sheria.


Wakili Marenga amesema kumekuwepo na jitihada kubwa kisheria kutaka maboresho ya Sheria lakini changamoto hata pale kesi zinapotolewa maamuzi  Serikali haitekelezi.


Mkutano  huo wa Wadau na kuhusu Mikakati ya Utetezi wa Utawala wa Sheria, Nafasi ya Kiraia na Marekebisho ya Sheria Nchini Tanzania umeandaliwa  mashirika manne.


Mashirika hayo ni Mtandao wa watetezi wa haki za binaadamu (THRDC), Chama cha Mawakili Tanganyika (TLS) chama chamawakili Afrika ya Mashariki, Chama cha Mawakili Zanzibar (ZAFELA) na Chama cha  Mawakili wa Pan Afrika (PALU) chini ya mradi wa Kulinda Utawala wa Sheria, Nafasi ya Kiraia na Uwajibikaji Tanzania kupitia Ushirikiano na Ubia Ulioboreshwa ( SCATZ) na unafadhiliwa na Jumuiya ya Ulaya.


Mwisho

No comments: