NMB yatoa elimu ya fedha kwa wafanyabiashara Moshi - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Sunday, 28 June 2026

NMB yatoa elimu ya fedha kwa wafanyabiashara Moshi

 

Baadhi ya wafanyabiashara mkoani Kilimanjaro wakipewa elimu mbalimbali ya umuhimu wa kutunza na kuhifadhi fedha na Benki ya NMB.





Na Mwandishi wetu, Kilimanjaro


maipacarusha20@gmail.com 


Moahi. Benki ya NMB imekutana na wafanyabiashara wa Mkoa wa Kilimanjaro kwa lengo la kuwapa elimu ya fedha, kuwaeleza fursa mbalimbali zinazopatikana ndani ya benki hiyo pamoja na kuhamasisha utamaduni wa kuweka akiba ili kukuza biashara zao.


Akizungumza katika mkutano wa NMB Business Club uliowakutanisha wafanyabiashara mbalimbali mkoani Kilimanjaro,  Meneja Mwandamizi wa Idara ya Biashara wa NMB Makao Makuu, Leonard Tony, alisema benki hiyo imewakutanisha wateja, wadau na wateja watarajiwa kwa lengo la kuwafahamisha huduma, bidhaa na maboresho mbalimbali yanayoendelea kutolewa na benki hiyo.



Alisema moja ya maeneo waliyojikita kuyazungumzia ni umuhimu wa wafanyabiashara kuweka akiba kwenye akaunti zao, hatua inayosaidia benki kutathmini mwenendo wa biashara zao na kurahisisha upatikanaji wa mikopo pamoja na usimamizi wa marejesho.


"Akiba huwasaidia wafanyabiashara kujenga historia nzuri ya kifedha ambayo hutuwezesha kutambua uwezo wa biashara zao na kurahisisha utoaji wa mikopo pamoja na marejesho kwa wakati," alisema Tony.


Aliongeza kuwa NMB inaendelea kutoa elimu kuhusu namna bora ya kuendesha biashara, kutunza kumbukumbu za kifedha na kufuata sheria na taratibu za nchi ili biashara ziwe endelevu.


Kwa upande wake, msambazaji wa Taifa Gas Mkoa wa Kilimanjaro, Maria Olomi, alisema ushirikiano wake na NMB umechangia kwa kiasi kikubwa ukuaji wa biashara yake tangu alipoianzisha.


"Nimekuwa mteja wa NMB tangu nilipoanza biashara. Benki hii imenikuza na kunifikisha hapa nilipo. Tumekuwa tukipata mikopo yenye riba nafuu ambayo imetusaidia kupanua biashara zetu. Kwetu sisi, NMB ni benki rafiki," alisema.


Naye mfanyabiashara wa Moshi, Gidan Parma, alisema NMB imekuwa mshirika muhimu wa wafanyabiashara wa makundi mbalimbali kwa kuwawezesha kupata mitaji kupitia mikopo.


"Benki ya NMB ina mchango mkubwa kwa wafanyabiashara wadogo, wa kati na wakubwa. Kupitia huduma zake za mikopo imewawezesha wajasiriamali wengi kukuza biashara zao na kuongeza kipato," alisema.


Alisema huduma zinazotolewa na benki hiyo zimekuwa zikiwanufaisha wananchi wengi na kuchochea ukuaji wa biashara katika mkoa huo.


Mwisho.

No comments: