Serikali yatangaza mkakati kupunguza ukali wa maisha - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 11 June 2026

Serikali yatangaza mkakati kupunguza ukali wa maisha

 



Waziri wa Fedha, Balozi Khamis Mussa Omar amewasilisha mapendekezo ya hatua mpya za kodi kwa mwaka 2026/27 akisema yatajibu maswali na kukidhi kiu ya wananchi, wafanyabiashara na wawekezaji kwa kuweka sera zinazochochea uwekezaji, uzalishaji na kulinda viwanda.


Dkt Omar amesema hatua hiyo itawezesha Taifa kuchangia katika kufikia malengo ya Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.


Waziri Omar ameeleza hayo leo Alhamisi Juni 11,2026 wakati akiwasilisha mapendekezo ya bajeti kuu ya Serikali kwa mwaka 2026/27 bungeni jijini Dodoma, tukio linalofuatilia mubashara na Rais Samia Suluhu Hassan.


Kwa mujibu wa Balozi Omar, maboresho hayo pamoja na mambo mengine, yanalenga kukuza uchumi, kuongeza fursa za ajira na hatimaye kupunguza ukali wa maisha ya wananchi.

“Aidha, hatua hizo zinalenga pia kuimarisha usimamizi, ukusanyaji wa mapato ya ndani na kudhibiti upotevu wa mapato ya Serikali,” amesema Balozi Omar. 

Mbali na hilo, Balozi Juma amesema Serikali imekuwa ikiyafanyika kazi kina maoni yaliyotolewa na Tume ya Rais ya Maboresho ya Mfumo wa Kodi, mapendekezo ya kurekebisha mfumo wa kodi kwa mwaka 2026/27 yamezingatia baadhi ya 49 maoni hayo. 

Ametaja baadhi ya maeneo yanayopendekezwa kufanyiwa maboresho ni kustawisha sekta za uzalishaji katika mnyororo wa thamani wa mafuta ya kula, hatua itakayowezesha msamaha wa kodi ya ongezeko la thamani kwenye mafuta ya kula yaliyozalishwa kwa kutumia mbegu zinazozalishwa ndani ya nchi.

Balozi Omar amesema hatua nyingine ni mnyororo wa pamba, nguo na vitambaa, jambo litalowezesha nafuu wa ushuru wa forodha kwenye malighafi, mashine vinavyotumika katika vitambaa na nguo nchini na uzalishaji vipuri.

No comments: