![]() |
Queen Lema,Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mwanariadha maarufu Alphonce Simbu amefanikiwa kulitembelea Banda la ZARA Tanzania Adventure kwenye maonesho ya Kili Fair huku akisema kuwa ZARA imekuwa na mchango mkubwa sana hasa kwenye sekta ya Utalii hapa nchini.
Simbu ambaye aligeuka kivutio kwenye Maonesho ya Kili Fair yaliyofanyika katika viwanja vya Magereza Kisongo alionesha nia yake ya kuipongeza sana Kwa kuwa mstari wa mbele kwenye sekta ya utalii
Simbu alisema kuwa pamoja na kuwepo kwa Summit Run Challenge ndani ya maonyesho ya Karibu-KiliFair Bado wadau hao wameweza kuwa kiungo kizuri kati ya Taifa na Taifa hasa kwenye sekta ya utalii na wadau wengine wa michezo wanatakiwa kuiga mfano huo
"Mimi nawapenda sana ZARA wamekuwa wadau wakubwa kwenye sekta ya utalii lakini Leo ndio wadhamini hii ni nzuri sana na inahamasisha sana nawasihi na wengine wasiache kuiga mfano huo"aliongeza
Simbu amesema juhudi za ZARA Tanzania Adventures katika kuitangaza Mlima Kilimanjaro na vivutio vingine vya utalii zimeendelea kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kama moja ya destinasheni bora za utalii.
Katika hatua nyingine Afisa Masoko wa Zara Tanzania Adventures, Nancy Ngotea, amepongeza shindano hilo la "Summit Run Challenge" akilitaja kama ubunifu mkubwa unaounganisha sekta ya michezo na utalii kwa mafanikio. Alieleza kuwa changamoto hiyo imevutia wageni wengi wa ndani na nje ya nchi, huku ikitoa jukwaa zuri la kuonyesha uwezo wa utalii wa Tanzania duniani kote.
Ngotea pia alipongeza jitihada za serikali chini ya Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuimarisha utangazaji wa utalii ndani na nje ya nchi, jambo linalofanya sekta hiyo kuendelea kukua.
Hataivyo katika kipindi chote cha maonyesho hayo ambapo wageni wengi walichuana vikali kupanda mfano wa Mlima Kilimanjaro uliowekwa uwanjani hapo.

No comments:
Post a Comment