Waziri Nanauka awataka viongozi wa dini kuwa mabalozi wazuri wa amani ya nchi - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 9 June 2026

Waziri Nanauka awataka viongozi wa dini kuwa mabalozi wazuri wa amani ya nchi

 




Na Mwandishi wetu,Meru


maipacarusha20@gmail.com



Waziri wa nchi, Ofisi ya Raisi -Maendeleo ya Vijana, Joel Nanauka amewataka viongozi wote wa dini nchini kuhakikisha kuwa wanatangaza na kuhubiri injili ambayo Haina ubaguzi wa dini.


Nanauka aliyasema hayo wiki iliopita katika maafali ya 57 ya chuo Cha biblia Cha sakila, kilichopo chini ya Kanisa la international Evangelism church.


Alisema kuwa ili amani ya dini na Taifa liweze kuharibika ni lazima viongozi wa nyumba za ibada waweze kwenda kuwa waharibifu wa amani ya nchi 


Aliongeza kuwa viongozi wa dini Wana nafasi kubwa sana katika kuhakikisha kuwa wanaacha kuhubirj injili yenye vichochea vya uharibifu wa amani ya nchi


"Ukiwa kiongozi wa dini hakikasha unakuwa balozi mzuri wa kuhubiri amani, amani ya Tanzania inatakiwa itunzwe Tena kwa gharama kubwa sana"aliongeza


Katika hatua nyingine aliwataka viongozi wa dini waweze kuhakikisha kuwasimamia ipasavyo maadili ya nchi kupitia kwenye mibara na madhabau yao 


Nanauka alisema viongozi wa dini wanapohubiri umuhimu wa maadili mema kwenye jamii inasaidia sana kupunguza Kasi ya mambo mabaya na matukio makubwa.


"Tuangalie sasa ivi mmonyoko wa maadili jinsi ulivyo mkubwa lakini matukio makubwa ambayo yanatokea Tena hasa Mauaji jamani tusikae kimya na tusikubali kabisa hili tuhubiri amani, pamoja na upendo"aliongeza 


Naye Askofu mkuu wa Kanisa Hilo hapa nchini Dkt Eliud Isangya alisema kuwa kanisa lao halipingani na Serikali Bali linatumia muda wao mwingi kuiombea Serikali 


Isangya alisema kuwa Tanzania ni nchi ya amani ambayo Ina asali nyingi pamoja na Maziwa hivyo basi inatakiwa kutunzwa sana.


"Leo tunawaitimu hapa mbele yetu napenda kuwapongeza sana lakini waende wakahubiri amani na upendo, tuhakikishe kwa umoja wetu tunaulinda amani ya nchi"aliongeza.


Alihitimisha kwa kuwataka watanzania nao kukataa kuwa wakimbizi kwenye nchi yao Bali wanatakiwa kutumia muda wao mwingi kuiombea Serikali


Nao wahitimu walisema kuwa wanashukuru chuo hicho kuwa sehemu ya mafanikio yao lakini pia wanashukuru viongozi  wa Serikali kuwa pamoja na wao katika majira yote


Walisema pamoja na shukurani hizo Bado wanakabiliwa na changamoto ya ubovu wa barabara ya kutoka Kikatiti mpaka chuoni Hapo  hivyo basi wanaiomba Serikali kuweza kutatua tatizo Hilo ambalo limedumu kwa muda mrefu sasa


Mwisho

No comments: