Askari wanyapori Babati wapatiwa mafunzo ya huduma za Kwanza na Ulinzi kutoka Jeshi la Marekani. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 27 July 2026

Askari wanyapori Babati wapatiwa mafunzo ya huduma za Kwanza na Ulinzi kutoka Jeshi la Marekani.

 




Mwandishi wetu.


maipacarusha20@gmail.com 


Askari 49 wa wanyamapori katika eneo la hifadhi ya Jamii ya Wanyapori ya Burunge,wilaya ya Babati Mkoa wa Manyara wamepatiwa mafunzo ya utoaji huduma ya kwanza Kwa watalii na jinsi ya kufanya Doria ya kupambana na majangili.


Mafunzo hayo ya siku nne yametolewa na wanajeshi wa kikosi cha Anga wa Marekani kupitia ubalozi wao hapa Tanzania, Kwa uratibu wa Taasisi ya uhifadhi Chem chem association ambayo imewekeza shughuli za Utalii katika eneo hilo.




Akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo, Mkuu wa ldara ya Maendeleo ya Jamii halmashauri ya Babati, January bikubwa amesema  mafunzo hayo yameongeza uwezo Kwa askari hao kutumikia jamii.


Amesema Askari hao sasa wanatarajia kutoa huduma bora kwa watalii na wananchi wanaoishi jirani na hifadhi hiyo.



Afisa wanyapori wilaya ya Babati Beatrice Onesmo ameeleza kuwa Askari hao pia wamefundishwa njia bora za kufanya Doria.


"Askari hao wamekuwa na mbinu za Kisasa za Doria na hivyo kukabiliana na ujangili"amesema



Mmoja wa wakufunzi Askari wa Jeshi la Anga la Marekani Captain Benjamin mccall anazungunzia mafunzo hayo amesema yatawasaidia Sana Askari kuboresha Utendaji wao.


"Tunaimani uwezo wao wa kutoa huduma ya kwanza umeimarika lakini pia uwezo ea kukabiliana na ujangili"amesema 

Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Chem Chem , Clever Zulu 



Mtendaji Mkuu wa Taasisi ya Chem Chem , Clever Zulu  anasema wameratibu mafunzo hayo ili kuboresha Utendaji wa Askari.


Amesema lengo la Chem chem Ni kuzifanya hifadhi ya Burunge kuwa ya kipekee barani Afrika Kwa kutoa huduma Bora Kwa watalii lakini pia kuwepo na wanyapori wengi zaidi.


"Mafunzo haya pia yataongeza mapato ya Serikali katika utalii kwani SASA watalii WA hadhi ya juu watafika Burunge WMA kwani Ni eneo bora na salama"amesema 


Mmoja wa washiriki wa mafunzo hayo, Fatuma seleman anazungumza walichojifunza alisema kimewasaidia kuboresha Utendaji Kazi wao.



Mafunzo hayo ya siku nne yalishirikisha   Askari 49 yalitolewa na Askari wa kikosi cha Anga cha Jeshi la Marekani kupitia ubalozi wa Marekani hapa Nchini.ikiwa ni mfululizo wa mafunzo Kwa askari WA hifadhi katika eneo hilo awali walifundishwa pia matumizi ya technolojia za Kisasa za Ulinzi,ukamataji watuhumiwa,upelelezi na uandaaji wa mashitaka.


Mwisho



No comments: