BARAZA LA VYAMA VYA SIASA: MARIDHIANO YAONGOZWE NA SERIKALI KWA MASLAHI YA TAIFA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 23 July 2026

BARAZA LA VYAMA VYA SIASA: MARIDHIANO YAONGOZWE NA SERIKALI KWA MASLAHI YA TAIFA

 



Mwenyekiti wa baraza la vyama vya siasa Juma Ali Khatibu

Mwenyekiti wa chama cha AAFP, Said Sudi Said


Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com


BARAZA la Vyama vya Siasa Tanzania limesema mchakato wa maridhiano unapaswa kuongozwa na Serikali kwa kuwa ndiyo yenye mamlaka ya kuyasimamia, huku likisisitiza umuhimu wa wadau wote kukaa pamoja ili kuimarisha umoja, demokrasia na maslahi mapana ya Taifa.


Mwenyekiti wa Baraza la Vyama vya Siasa Tanzania,Juma Ali Khatibu, alisema hayo wakati akizungumza na waandishi wa Habari baada ya kukamilika kwa uchaguzi wa viongozi wa baraza hilo,mjini Morogoro.


Khatibu ambaye Mwenyekiti wa taifa wa chama cha ADA-TADEA alisema kuwa huwezi kufanya maridhiano ya mtu wa kutoka nje ya Tanzania na ambaye si mwenye serikali na alimpongeza  Rais Dk Samia Suluhu Hasaan kwa kuleta fikra ya maridhianio ni jambio jema na ni zuri.


Hivyo aliwataka watanzania kuendelea kushikamana na kufanya siasa zenye kujenga nchi  na zenye kuunganisha wananchi  na kuachana na kufanya siasa za kuwagawa na kuwagombanisha .


Khatibu aliwashauri wanasisa wasitegemee hoja ya maridhiano ziwe kama mtaji wa kisiasa kwani jambo hilo halipendezi  kwa mtakabali wa Taifa letu ,bali  hoja ya mardhiano ni kuweka siasa safi, uongozi bora, ushirikiano na kufungua demokrasia pana zaidi.


Licha ya  maridhiano alisema baraza pia litajikita kufanya kazi ya kuona ni miradi gani ya maendeleo ili kuishauri Serikali iyafanyie kazi  kwa ajili ya kuongeza  mapato ya kwa maslahi mapana ya wananchi.

Katibu Mkuu UDP, Saumu Rashid

Kuhusu mikutano ya hadhara iliyozuiwa alisema  Baraza la Vyama vya Siasa limepanga kuishauri Serikali kuhusu zuio la mikutano ya hadhara kuwa ni vyema sasa ikaangalia upya zuio hilo kwani limeumiza vyama vingine ambavyo havijafanya kosa .


Alisema Baraza litaishauri  Serikali iangalieupya uamuzi wake  kwani vyama vya siasa vipo 19 na kwamba kikitokea chama kimoja kimevunja sheria ya vyama vya siasa  au kimevunja sheria za nchi  visihukumiwe vyama vyote  bali ahukumiwe mtu na kile chama kilochofabnya kosa ili  kulinda misingi ya demokrasia  na haki ya Vyama vya Siasa hapa nchini.


“Kile chama ambacho kimevuja sheria kimefanya makosa au viashiria vya kufanya vurugu aadhibiwe mtu binafsi na Chama chake, visiadhibiwe vyama vingine  ambavyo havijahusika na n makosa yale,"alisema Khatibu.


Kuhusu uchaguzi wa Mwenyekiti wa Baraza pamoja na Makamu Mwenyekiti,wajumbe waliendelea kumwamini na kumchangua kwa mara nyingine tena,Khabitu kwa kura 30  kati ya 31 zilizopigwa na kura moja ikiharibika na kumwezesha kuongoza kipindi kingine cha uongozi wa miaka miwili.


Pia walimrejesha tena kwenye nafasi ya Makamu wa Baraza hilo  , John Mongella ambaye ni Naibu Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) Bara kwa kumpingia kura 30 za ndiyo kati ya 31 na moja ya hapana.


Naye Katibu Mkuu wa Chama cha UDP na Mjumbe wa Baraza hilo, Saum Rashid alisema kuwa tunapokuza demokrasia ndani ya nchi yetu tunadumisha amani  na utulivu.


“Kama ni kiongozi wa mwanamke niwaase watanzania tueendelee kudumisha amani na utulivu wan chi yetu , tutatue changamoto zetu wa mazungumzo sisi wenyewe na kufikia muafaka,”alisema Saum.


Mwenyekiti wa Chama cha  Wakulima (AAFP ).Taifa, Said Sudi Said alisema watanzania wanaouwezo wa kutatua matatizo yao wenyewe pasipo kutegemea mtu wa kutoka mataifa ya nje na hilo limewahi kufanywa na Baba wa Taifa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliyekuwa msuluhushi wa migogoro katika nchi kadhaa za kiafrika .


Mwisho.

No comments: