![]() |
| Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Dkt Johannes Lukumayi akisikiliza kero za wananchi wa Mwandeti |
maipacarusha20@gmail.com
Mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Dkt Johannes Lukumayi ametembelea vijiji mbalimbali vya kata ya mwandeti, pamoja na Musa, na kisha kukagua miradi mbalimbali ya maendeleleo inayotekelezwa na Serikali
Mbali na mbunge huyo kufanya ziara katika kata hizo pia mbunge huyo amesikiliza na kutatua changamoto mbalimbali zilizopo kwenye kata hizo
Akiongea na maelfu ya wananchi waliodhuria katika mikutano ya hadhara ya mbunge huyo alisema kuwa mara baada ya kuchaguliwa na wananchi alipata pia ridhaaa ya kuwa na nyadhifa mbalimbali za bunge la Jamuhuri ya muungano wa Tanzania
Aliwashukuru wananchi wa mwandeti kwa kuweza kumpatia kura nyingi yeye pamoja na Raisi Samia suluhu pamoja na diwani wa kata hiyo
Alisema kuwa kupitia kura nyingi Sana ambazo zimetoka kwenye kata ya Mwandeti alisema Serikali itaendelea kuboresha miradi mbalimbali hasa ya kijamii
Dkt Lukumay alisema kuwa mwandeti pamoja na Musa ina wananchi wengi ambao wanajitoa sana kwenye masuala ya maendeleleo na hivyo yeye atahakikisha kuwa anasimamia maitaji yote ndani ya kata hiyo
![]() |
| Wakazi wa kata ya Mwandeti wakimsikiliza mbunge wa Jimbo la Arumeru Magharibi Dkt Johannes Lukumayi |
Pia aliwataka watalaamu wa sekta mbalimbali ambao wameajiriwa na Serikali wanatakiwa watembelee miradi na kisha kubaini changamoto mbalimbali ambazo zinasababisha miradi hiyo kushindwa kukamilika kwa wakati
Alihitimisha kwa kuwataka wananchi washirikiane kuleta maendeleo bila itikadi ya kisiasa lakini pia kushirikiana na wawekezaji ambao wanawekeza miradi mbalimbali ndani ya Kata hiyo
Nao wananchi wa kata hiyo walisema kuwa wanaiomba Serikali iweze kuwatatulia matatizo mbalimbali ambayo yanawakabili
Waliomba kuboreshewa zaidi kwenye sekta ya afya,elimu pamoja na miundombinu ambayo ni muimu kwenye sekta ya maendeleo hapa nchini
Mwisho





No comments:
Post a Comment