![]() |
| Kiongozi wa Mwenge Kitaifa Ndugu Wazo Michael Mwango'nda akikagua daraja la Masagi akiangalia kama limekidhi viwango vya Ujanzi |
SEIF TAKAZA, IRAMBA
maipacarusha20@gmail.com
KIONGOZI wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Kitaifa mwaka 2026, Wazo Michael Mwang'onda, ametoa wito kwa wananchi wa Iramba kuitunza miradi ya maendeleo inayotekelezwa na serikali.
Wito huo umetolewa tarehe 24 Julai, 2026, alipokua akizindua daraja la Masagi lililopo katika barabara ya Kibigiri–Masagi–Tyeme, kata ya Mtoa.
" Tuitunze miradi hii ikawe na manufaa kwa kizazi cha sasa na cha baadae" Alisema
Daraja hilo ni miongoni mwa miradi ya maendeleo iliyotembelewa na Mbio za Mwenge wa Uhuru mwaka 2026, likiwa linatekelezwa kwa lengo la kuboresha miundombinu ya usafiri na usafirishaji pamoja na kurahisisha utoaji wa huduma kwa wananchi.
Mradi huo umegharimu shilingi 963.2 na umekamilika ukihusisha ujenzi wa daraja lenye urefu wa mita 20 na upana wa mita 5.5, ujenzi wa kuta za kuimarisha na kulinda daraja, pamoja na uboreshaji wa barabara ya maingilio ya daraja.
Kukamilika kwa daraja la Masagi kumeimarisha mawasiliano ya barabara ndani na nje ya Kata ya Mtoa, kurahisisha usafiri na usafirishaji wa watu, na bidhaa mbalimbali, kuongeza fursa za biashara na uwekezaji, pamoja na kuboresha upatikanaji wa huduma za kijamii, aidha, mradi huo unatarajiwa kuchochea ukuaji wa shughuli za kiuchumi na kuinua ustawi wa wananchi wa kata ya Mtoa na maeneo jirani.


No comments:
Post a Comment