![]() |
| mkuuu wa mkoa wa Arusha CPA Amoss Makalla Ameagiza mradi wa stand mpya kukamilika kwa wakati |
![]() |
Mwandishi Wetu, maipac
maipacarusha20@gmail.com
Mkuu wa mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amebainisha kuwa kukamilika kwa mradi wa ujenzi wa Kituo cha mabasi mkoa wa Arusha, kutapunguza changamoto ya msongamano wa magari katikati ya Jiji la Arusha na kuweka wazi kuwa wajibu wa Serikali ni kusimamia ili mradi huo ukamilike kwa wakati.
Mhe. Makalla amesema hayo leo Jumanne Julai 28, 2026, wakati wa ziara yake ya kikazi ya kukagua maendeleo ya utekelezaji wa mradi huo unaotekelezwa kwenye Kata ya Muriet kwa gharama ya shilingi Bilioni 14.3, fedha kutoka Serikali kuu, kupitia mradi wa uendelezaji Miji Tanzania TACTIC.
"Stendi hii ni muhimu kwa wakazi wa Arusha, kukamilika kwakwe mwezi Novemba 2026, kunatarajiwa kupunguza foleni katikati ya Jiji pamoja na kurahisisha usafiri na usafirishaji wakati wa michuano ya AFCON inayotarajiwa kufanyia mkoani Arusha mwaka 2027". Amesisitiza CPA Makalla.
Awali, Mhe. Makalla amemtaka mkandarasi mzawa anayetekeleza mradi huo M/S Mohammed Bulders Ltd, kuongeza kasi ya ujenzi ili mradi huo ukamilike kwa wakati kulingana na mkataba ili wananchi wa Jiji la Arusha wanufaike na mradi huo.


No comments:
Post a Comment