Mussa Juma
maipacarusha20@gmail.com
Makamu wa Rais wa Jamuhuri ya Muungano WA Tanzania Dr. Emmanuel Nchimbi Kesho Julai 24,2026 anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika mkutano mkuu wa mtandao wa Mashirika ya watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC) .
DK Nchimbi anakuwa kiongozi wa Pili mkubwa Nchini kuhudhuria mkutano huo kwani tayari Rais Samia Suluhu Hassan pia aliwahi kuwa mgeni rasmi.
Akizungumza na MAIPAC Media Tanzania, Mratibu wa Taifa wa THRDC, Wakili Onesmo ole Ngurumwa Leo Julai 23,2026, amesema maandalizi yote muhimu ya mkutano huo yamekamilika.
Ole Ngurumwa amesema mkutano huo, utafanyika katika ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.
Amesema wanachama wa THRDC, Zaidi ya Mashirika 150 wanatarajia kushiriki Mkutano huo katika ukumbi huo na kupitia mtandao ya kijamii.
"Ni mkutano wetu wa kawaida wa kila mwaka ambapo tunatarajia kutoa pia taarifa ya hali ya watetezi wa Haki za Binadamu nchini na taarifa nyingine za tafiti za masuala mbali mbali ambayo yanahusu Jamii"amesema
Ole Ngurumwa amesema mkutano huo pia utahudhuriwa na wadau mbali mbalimbali wa Haki za Binadamu.
Wakizungumzia mkutano huo baadhi ya wanachama wa THRDC walieleza miongoni mwa mambo ambayo wanatarajia yatazungumzwa ni pamoja na kutungwa Sheria ya kuwalinda watetezi wa Haki za Binadamu na kuondoa dhana potofu kuwa ni wachochezi katika Jamii.
Mwisho

No comments:
Post a Comment