Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amekitaka Chama cha Mawakili wa Serikali kuongeza weledi kuhusu matamko na taratibu za kimataifa, akitaka kuyaangalia na kuyatafsiri kwa uharaka na kutoa majawabu ili kuhami uhuru wa nchi.
Dkt Samia ameeleza hayo leo Jumatatu Julai 13,2026 akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), Julai 13, 2026.
“Ni wajibu wenu na kuyatilia manani kwa kugundua viashiria mapema, kushauri kwa wakati, kwa usahihi na kwa njia njema. Jukumu lenu pia kuhakikisha nchi inalindwa na kusimamiwa kwenye misingi imara ya kisheria
Ameongeza kuwa.” Sheria tunazozitunga, na tunazotarajia kuzitunga kulinda uhuru wetu, haki za raia na rasilimali za Taifa letu. Mwanasheria au wakili wa Serikali hapimwi kwa kesi alizoshinda, bali kwa migogoro aliyoizuia, fedha za umma alizoziokoa na makosa aliyoyazuia kabla ya hajaharibu Taifa,” ameeleza Dkt Samia.
Mbali na hilo, Samia amesema ofisa wa sheria wa Serikali anapimwa pia kwa uwezo wa kutafsiri sheria na matamko ya kimataifa kwa kujidhatiti kuihami nchi na vitishio vya ndani au nje ya Taifa.
“Pamoja na kutusaidia katika shughuli za maendeleo na ustawi wa watu wetu, sheria zetu zinapaswa kuwa kinga dhidi ya viatarishi ya uhuru na ustawi wa Taifa letu,” amesema Samia.

No comments:
Post a Comment