Rais wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan amesema kazi yake ni kulea vyama vyote vya mawakili vya Serikali na binafsi kikiwemo Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS), kinachongozwa na Boniface Mwabukusi.
Dkt Samia ameeleza hayo leo Jumatatu Julai 13,2026 akifungua Mkutano Mkuu wa Chama cha Mawakili wa Serikali katika Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa wa Arusha (AICC), Julai 13, 2026.
“Kazi yangu kama mkuu wa nchi ni kulea vyama vyote, nawalea nyie wa Serikali na kina Mwabukusi mawakili binafsi. Wakina Mwabukusi walikuja kuniona na changamoto zao nimeanza kuzifanyia kazi kwa kupeleka magari mawili ili kuunga nguvu kwenye Samia legal campaign.
“Mambo mengine wameomba nitayatekeleza polepole,” amesema Dkt Samia.
Dkt Samia ameahidi kukiendeleza na kukiwezesha chama cha mawakili wa Serikali ili kitekeleza majukumu yake vizuri.
![]() |



No comments:
Post a Comment