MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA IRAMBA TAYARI KUMULIKA MIRADI YA MAENDELEO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 24 July 2026

MWENGE WA UHURU WAPOKELEWA IRAMBA TAYARI KUMULIKA MIRADI YA MAENDELEO

 


 SEIF TAKAZA IRAMBA


maipacarusha20@gmail.com 


Mwenge wa Uhuru umewasili katika Wilaya ya Iramba ukitokea Halmashauri ya Manispaa ya Singida na kupokelewa rasmi na Mkuu wa Wilaya ya Iramba, Alhaj Suleiman Mwenda kutoka kwa Mkuu wa Wilaya ya Singida  Godwin Gondwe


Makabidhiano hayo ya Mwenge wa Uhuru yamefanyika tarehe 24 Julai, 2026 katika Uwanja wa Mcharukoni uliopo kijiji cha Ndulungu.


Akipokea Mwenge wa Uhuru, Alhaj Mwenda amesema kuwa Mwenge wa Uhuru utakimbizwa umbali wa kilometa 174.5 ndani ya Wilaya ya Iramba na utapitia jumla7 ya miradi nane (8) ya maendeleo yenye jumla ya thamani ya shilingi bilioni 12.5. kati ya miradi hiyo, minne (4) itazinduliwa, mitatu (3) itawekewa mawe ya msingi, huku mradi mmoja (1) ukitembelewa na kukaguliwa.

No comments: