RC MAKALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPANI NCHINI TANZANIA - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Friday, 24 July 2026

RC MAKALLA AFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA JAPANI NCHINI TANZANIA

 

 


Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amekutana na Balozi wa Japani nchini Tanzania, Mhe. Balozi Mikami Yoichi, alipomtembelea ofisini kwake leo Alhamisi Julai 24, 2026.


Mhe. Balozi na Mkuu wa mkoa wa Arusha, mazungmzo yamelenga kuendelea kuimarisha ushirikiano baina ya nchi hizo mbili, ushirikiano ambao ulijengeka kwenye misingi imara tangu enzi na enzi. 


Mhe.Makalla ameweka wazi kuwa Tanzania na Japani ni marafiki wa kihistoria tangu enzi za Serikali ya awamu ya kwanza, chini ya Hayati Mwl. Julias Kambarage Nyerere, ushirikino ambao umedumu kwa misingi ya viongozi wa nchi hizo mbili huku akimshukuru Balozi Yoichi kwa miradi mingi ya maendeleo kisekta, inayotekelezwa nchini kupitia ubalozi wa Japani.


Aidha, CPA Makalla ametumia fursa hiyo kuelezea fursa za kiutalii zinazopatikana Arusha, kwa kuwa Arusha ni kitovu cha utalii pamoja na kumkaribisha yeye na Wajapani wote kutembelea vivutio vya utalii vinavyopatikana Arusha, ambapo watafurahia mandhari inayovutia, inayoambatana na hali ya hewa nzuri pamoja na ukarimu wa wakazi wa mkoa huo. 


Aidha, Katika mazungumzo yao Mhe. Makalla na Balozi Yoichi wamekubaliana kuendeleza ushirikiano baina ya Tanzania na Japani kwa maendeleo ya nchi hizo kwa maslahi ya wananchi wa pande zote mbili.


Awali, mazungumzo yao pia yamelenga kufanikisha wabunge wa Japani kuhudhuria kwenye Mkutano wa *Bunge ya Dunia - IPU mkutano unaotarajia kufanyika Jijini Arusha mapema mwazi Oktoba mwaka huu wa 2026*.

No comments: