![]() |
Rais Samia Suluhu Hassan amezindua meli nne mpya za mizigo zenye uwezo wa kubeba tani 2,000 kila moja katika hafla ya kitaifa iliyofanyika leo, Julai 20, 2026, katika Bandari ya Kigoma, hatua inayolenga kuongeza ufanisi wa usafirishaji wa mizigo na kuimarisha biashara katika ukanda wa Ziwa Tanganyika.
Meli hizo zimetengenezwa na kampuni ya Gold Voyage Logistics Limited kutoka China na zinatarajiwa kutoa mchango mkubwa katika usafirishaji wa mizigo kati ya Tanzania na nchi jirani za Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DRC), Burundi na Zambia kupitia Ziwa Tanganyika.
Uzinduzi huo unaenda sambamba na mkakati wa Serikali wa kuifanya Kigoma kuwa lango kuu la biashara kuelekea masoko ya Afrika ya Kati kupitia uboreshaji wa usafiri fungamanishi unaojumuisha reli, bandari na usafiri wa majini, kwa mujibu wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.


No comments:
Post a Comment