Rais Samia kuzindua ujenzi wa SGR Tabora–Kigoma leo - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 20 July 2026

Rais Samia kuzindua ujenzi wa SGR Tabora–Kigoma leo

 



Rais Samia Suluhu Hassan leo Julai 20, 2026 anazindua na kuweka jiwe la msingi la ujenzi wa Reli ya Kisasa (SGR) kutoka Tabora hadi Kigoma.


Mradi huo wa kilometa 506 wenye thamani ya Sh trilioni 6.31 utajengwa ndani ya miezi 48 hadi mwaka 2030 na unatarajiwa kutoa ajira zaidi ya 15,000 kwa wakazi wa Tabora na Kigoma.


Aidha, reli hiyo itapunguza muda wa safari kutoka Dar es Salaam hadi Kigoma hadi saa saba au nane na kurahisisha usafirishaji wa mizigo kwenda Burundi na DRC.


Wachambuzi wa uchumi wanasema mradi huo utafungua fursa mpya za biashara, uwekezaji, viwanda na utalii, na kuifanya Kigoma kuwa kitovu muhimu cha biashara katika ukanda wa Maziwa Makuu.

No comments: