
Baraza Maalum la Madiwani la Hashauri ya Wilaya ya Iramba katika kikao cha Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali kilichofanyika Ukumbi Mkubwa wa Halamashauri ya Wilaya ya Iramba
SEIF TAKAZA – IRAMBA
maipacarusha20@gmail.com
MKUU wa Mkoa wa Singida Halima Dendego ameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Iramba, Mkoani Singida kwa ujasiri kufuta hoja za ukaguzi ambazo zilikuwepo kwa muda mrefu hadi kufikia hoja 23 zitokanazo na Miradi mbalimbali ya Maendeleo Wilayani Iramba.
Pongezi hizo zimetolewa leo katika kikao maalumu cha Baraza la Madiwani kilichofanyika katika ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba.
“Natoa pongezi za dhati kwa Mwenyekiti wa Halmashauri Innocent Msengi, Madiwani, watendaji wa halmashauri chini ya uongozi thabiti na Mkuu wa wilaya Alhaj Suleman Mwenda, lakini pia nimshukuru Rais Samia Suluhu Hassan Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kututeulia Mbunge wa Iramba Magharibi Dr. Mwigulu Lameck Nchemba, kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Tusimuangushe, Halmashauri hii iwe mfano wa kuigwa na halmashauri nyingine kwa kuwa Waziri Mkuu ametoka jimbo hili” alisisitiza Dendego.
Naye Mwenyekiti wa halmshauri hiyo Innocent Msengi amewaahidi watumishi na watendaji wote wa halmashauri kuongeza juhudi za ukusanyaji wa mapato ya ndani ili iweze kuvuka malengo iliyojiwekea kwa mwaka 2026/2027.
Akizungumza wakati wa mkutano maalum wa baraza la madiwani kupitia hoja za ukaguzi za Mdhibiti wa Mkaguzi wa Hesabu za serikali (CAG) kwa mwaka wa fedha 2024/2025.
“Ipo Miradi ambayo haijakamilika niwaombe viongozi wenzangu tuhakikishe tunasimamia miradi sehemu zetu ili miradi yetu ikamilike kama ilivyopangwa” Alisisitiza Msengi
Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri hiyo Michael Matomola amesema Halmashauri hiyo imejipanga kukusanya zaidi asilimia 33 ya mapato katika robo ya kwanza ya mwaka 2026/2027 sanjari na kudhibiti utoroshaji wa mazao ili kufanikisha malengo ya makusanyo kama ilivyopangwa na Halmashauri.
MWISHO
No comments:
Post a Comment