![]() |
| Mkuu wa Mkoa Arusha CPA Amoss Makalla akimsukuma Farida mwinyi (34) mkazi wa Njiro mara baada ya Kumkabidhi kitimwendo |
Mwandishi Wetu Maipac
maipacarusha20@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Arusha CPA Amoss Makalla amekabidhi vitimwendo 60 vyenye thamani ya shillingi millioni 35 kwa walemavu Mkoani Arusha.
Vitimwendo hivyo vimetolewa na Taasisi ya Wheelchair Foundations ya Marekani kwa ushirikiano wa Chem Chem Association na friedkin Conservation Fund(FCF).
Wanufaika wa vitimwendo hivyo ni walemavu waliopo katika Halmashauri za Arusha Jiji viti 30, Monduli 10, Arusha DC10 na Meru 10.
Akizungumza wakati wa ugawaji wa vitimwendo hivyo RC Makalla ameishukuru Chemchem association inayofanya kazi za uhifadhi na Utalii wa picha kwa kutoa msaada huo kwa kushirikiana na Friedkin Conservation Fund pamoja na wheelchair foundation toka Marekani
"Msaada huu utapunguza adha za watu Wetu wenye changamoto za ulemavu kuweza kutimiza majukumu Yao ya Kila siku na kuwezesha uzalishaji mali kwa manufaa ya familia, jamii na Taifa kwa ujumla" alisema Makalla
Nimewashukuru kwa msaada huu Mkubwa lakini pia nimewaomba waendelee kutusaidia vitimwendo vingine kwani mahitaji ya walemavu bado ni makubwa Mkoani kwetu
![]() |
Mapema Meneja Mkuu wa chemchem association Clever Zullu amesema kuwa wanashukuru Taasisi ya Wheelchair foundations toka Marekani kwa kutoa msaada huo kwa watu wa Arusha kwani utawasaidia katika kujikwamua kiuchumi. Zulu amesema msaada huo ni mfululizo wa viti ambavyo tayari vimetolewa mkoa wa Manyara na Mara kutokana na juhudi za wananchi kuendeleza uhifadhi.
![]() |
Aurelia Mtui Meneja miradi wa Friedkin conservation Fund amesema wamekuwa wakitoa msaada mbalimbali kwa jamii ikiwemo ya Afya, elimu na mazingira katika mikoa ya simiyu, manyara na kwa Sasa wameleta Arusha vitimwendo hivyo 60 vyenye thamani ya shillingi millioni 35
Rais wa Taasisi ya wheelchair foundation David Behrin amesema kuwa wanajivunia kutoa msaada wa vitimwendo hivyo ili kuchochea uchumi wa familia , jamii na Taifa kwa ujumla ambapo mpaka sasa wamekwishatoa vitimwendo 7000 Nchini Tanzania na wametoa container 7 zenye vitimwendo 260 kwa Taasisi ya Chemchem association vitagaiwa katika mikoa ya Manyara, Arusha na simiyu.
Baadhi ya wanufaika wa vitimwendo hivyo Sebastian Gabriel (50) mkazi wa Kisongo Halmashauri ya Arusha DC ameishukuru Chemchem, FCF na Wheelchair foundations kwa msaada huo kwani utamuwezesha kwenda katika shughuli zake za kusimamia kilimo kwa wakati tofauti na alivyokuwa akitumia magongo yaliyokuwa yanamchukulia muda mrefu kufika katika shughuli zake.
Farida mwinyi (34) mkazi wa Njiro Arusha ameishukuru sana CCA, FCF na Wheelchair foundations kwa msaada wa kitimwendo hicho kitamsaidia katika shughuli zake za Kila siku kuweza kutoka na kwenda katika shughuli kwani mwanzo ilikuwa lazima abebwe ili kutoka ndani mpaka nje katika usafiri, pia gharama za kukodisha bajaji Sasa zitapungua kwani ataweza kutumiakitimwendo hicho katika shughuli zake bila kulazimika kutaka msaada wa mtu mwingine.





No comments:
Post a Comment