![]() |
| Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Amoss Makalla Amshukuru Rais Samia kuwezesha barabara zote muhimu kwa ajili ya AFCON |
![]() |
Asema Barabara hizo zitaondosha foleni na kuchochea utalii |
Mwandishi Wetu, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Mkuu wa Mkoa wa Arusha Mhe. CPA Amos Gabriel Makalla amewataka wananchi wote waliolipwa fidia kwenye maeneo zinapojengwa barabara zote kwaajili ya maandalizi ya Michuano ya Mpira wa Miguu Mataifa ya Afrika - AFCON 2027, kuondoka ili kuruhusu Mkandarasi kuendelea na utekelezaji wa miradi hiyo.
Mhe. Makalla ametoa agizo hilo leo Julai 29,2026, alipotembelea na kukagua maendeleo ya ujenzi na upanuzi wa miundombinu ya barabara yenye urefu wa Km 9.1 kuanzia Makutano ya Ngarenaro - mzunguko wa Kisongo, Makutano ya Ngarenaro - Kona ya Nairobi na Makutano ya Ngarenaro - soko la Kilombero, kwa njia nne, mradi unaotekelezwa na Serikali kwa gharama ya shilingi Bilioni 87.9.
"Nimshukuru Mhe. Rais kwa kuwezesha ujenzi wa barabara hizi, niwaombe watalamu wasekta zote kutoa ushirikiano kuhakikisha hakuna kizuizi kwa Mkandarasi kufanya kazi, serikali ileshawalipa fidia wananchi wote kwa barabara zote za AFCON, zaidi ninawashukuru ambao wameshaondoka wameonesha uzalendo, na ambao hawajaondokaa niwaombe waondoke ili kupisha ujenzi ." Amesema Mhe. Makalla.
Aidha, CPA Makalla amebainisha kuwa, kukamilika kwa barabara hizo licha ya kuwa zitachochea shughuli za utalii na AFCON 2027 zaidi zitapunguza msongamano wa magari katika Jiji la Arusha.
Awali Meneja wa Wakala ya Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Arusha, Mhandisi Reginald Massawe amesema mradi huo wa barabara ya njia nne, utaondoa changamoto ya mafuriko katika maeneo ya Majengo, Shamsi na Ngarenaro kwa kujenga Mitaro mikubwa itakayopeleka maji kwenye Mto TANAPA.



No comments:
Post a Comment