Na Lilian Kasenene, Morogoro
maipacarusha20@gmail.com
Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais –Tawala za mikoa na Serikali za mitaa(TAMISEMI) anayeshughulikia Elimu, Atupele Mwambene, aliwataka walimu wa somo la Biashara kutumia fursa zilizopo katika maeneo yao na kuwa mfano wa ujasiriamali kwa wanafunzi, ili elimu wanayoifundisha ilete matokeo ya vitendo.
Mwambene alisema hayo mkoani Morogoro wakati akifunga mafunzo ya walimu 702 wa somo la Biashara mafunzo hayo yamefanyika Chuo Cha Ualimu Morogoro (Kigurunyembe).
Alisema walimu wanapaswa kuonyesha kwa vitendo namna elimu ya Biashara inavyoweza kutatua changamoto za maisha ya kila siku na kuchangia utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.
![]() |
Kwa upande wake, Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Elimu Tanzania (TET), Dk Aneth Komba, aliwahimiza walimu kutumia elimu na ujuzi walioupata kupitia mafunzo hayo kuboresha ufundishaji wa somo la Biashara, ili kuwajengea wanafunzi maarifa na stadi zitakazowasaidia kujitegemea.
Dk Komba alisema mafunzo hayo yalikuwa mahusisi kwa WALIMU wa shule za Sekondari za Serikali,lakini kama taasisi wanalenga pia kuwafikia walimu wa Sekondari kwa shule binafsi.
Naye Mwakilishi wa Educate, Nelson Musikula, alisema mafunzo hayo yameweka msingi imara wa kuleta mageuzi katika utoaji wa elimu ya Biashara kwa kuwajengea walimu uwezo wa kutumia mbinu za vitendo, hatua itakayochangia kuwaandaa wanafunzi kukabiliana na mahitaji ya dunia ya sasa.
Mwakilishi wa washiriki wa mafunzo hayo Mwalimu Chris Salapion alisema wao kama walimu wamepata maarifa,na mbinu mbalimbali za ufunfishaji wanafunzi,kuwajengea umahili wa kumudu stafi za ujuzi wa Karne ya 21.
Mwisho..

.jpg)

No comments:
Post a Comment