MKUU WA WILAYA IRAMBA AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MIRADI YA MAENDELEO - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 12 August 2026

MKUU WA WILAYA IRAMBA AWATAKA WANANCHI KUTUNZA MIRADI YA MAENDELEO

 

Mkuu wa Wilaya ya Irmba Mkoani Singida Alhaj Suleman Yusuph Mwenda akipewa maelezo ya Mradi kutoka kwa Mkandarasi anayetekeleza Mradi wa miji 28 ya mji wa kiomboi

SEIF TAKAZA, IRAMBA

maipacarusha20@gmail.com

Mkuu wa wilaya ya Iramba Alhaji Suleiman Yusufu Mwenda amewataka wananchi wa wilaya hiyo kulinda miraji ya maendeleo ili jamii ya sasa na ijayo ifaidi matunda yake.

Amesema hayo wakati wa ukaguzi wa utekelezaji wa mradi wa maji wa miji 28 katika mji wa kiomboi ambapo alimpongeza Rais Samia kwa jitihada zake za kuwaletea maendeleo wananchi wa Tanzania.

"Ndugu zangu wananchi wa kiomboi na kisana tuwaase vijana wetu waache kuharibu miundombinu ya serikali kwani  miradi hii inayotekelezwa sasa ni kwa manufaa yao na vizazi vijavyo hivyo wanapoharibu wanajiharibia wenyewe" Alisema

Mhandisi msimamizi wa mradi huo wa Megha Engineering  and Infrastructure (WAPCOS LTD) Basket Jafari toka nchini India amesema ghadi sasa wametekeleza mradi huo kwa asilimia tano tu kutokana na changamoto za vyanzo vya maji kutopatikana katika maeneo husika.

Kwa upande wake Mkurugenzi wa Mamlaka ya maji safi na usafi wa mazingira  KIUWASA Mhandisi Rashid Mwinjuma akitoa taarifa ya utekelezaji wa mradi huo amesema kuwa mradi huo ulisainiwa juni 6, 2022  na utekelezaji wake ulianza mwezi Aprili 2023 kwa gharama ya dola za marekani  12,782,721 ambazo ni sawa na shilingi za Tanzania 29,400,258,300.

Mhandisi huyo amesema kuwa kwa sasa ni asilimia tano tu za pesa hizo zimetumika  ambapo wanufaika wa mradi huo  ni watu 44,487 wa mji wa kiomboi.

 Mhandisi Mwinjuma amesema mkandarasi huyo ameahidi kukamilisha mradi huo mwezi Julai 2027 ambapo watajenga visitation nne zenye uwezo wa kuzalisha maji lita 103,000 kwa saa moja na pia watalaza mabomba ya vipenyo 100 - 300 kwa umbali wa kilomita 22 kutoka ulemo hadi igumo, kujenga kituo cha kusukuma maji kutoka visitation na ununzi wa gari moja aina ya Hilux Double cabin.

Mwenyekiti wa Bodi ya KIUWASA fredrich mpinga amemweleza mkuu wa wilaya kuwa changamotgo kubwa wanayoipata katika taasisi hiyo nimpamoja na madeni makubwa ambayo yanasababisha kuzorotesha utoaji wa maji inavyotakiwa.

"Mheshimiwa tunakuomba utusaidie kuwahaimiza taasisi za serikali ambazo mpaka sasaa tunazidai zaidi ya shilingi milion 20, ambapo madeni hayo yanasababisha tushindwe kufanya kazi kwa ufanisi" Alisema 

=/=

No comments: