NA SEIF TAKAZA IRAMBA
maipacarusha20@gmail.com
MKUU wa Wilaya ya Iramba, Mkoani Singida Alhaj . Suleiman Mwenda, ameipongeza Mamlaka ya Mapato (TRA) kwa kukusanya zaidi ya shilingi bilioni tano kwa mwaka wa fedha 2025 /2026 Wilayani Iramba.
Ametoa Pongezi hizo jana katika kikao kazi kilichofanyika katika Ukumbi wa Halmashauri ya Wilaya ya Iramba mjini Kiomboi.
Katika kikao hicho, Alhaj Mwenda amesema amefurahishwa na taarifa ya TRA baada ya kusikia imevuka lengo kwa kukusanya asilimia 122.7
“Ngugu zangu natoa pongezi za dhati kwa Watumishi wa TRA,kwani wamejitahidi katika ukusanyaji wa mapato hadi kuvuka lengo.” Alisema
Naiomba Halmashauri ya Wilaya hii ifanye kama wanavyofanya TRA ili Wilaya yetu iwe na mapato ya kutosha kwa ajili ya Maendeleo ya Wilaya yetu " Amesema Mwenda
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa Mapato TRA Wilaya ya Iramba Herel Peter Akyoo amesema lengo la Ukusanyaji mapato mwaka wa fedha 2025/2026 ilikuwa kukusanya shilingi bilioni 4,355,403,306.07
Kwa upande wake, Afisa Msimamizi wa Mapato TRA Wilaya ya Iramba Herel Peter Akyoo amesema lengo la Ukusanyaji mapato mwaka wa fedha 2025/2026 ilikuwa kukusanya shilingi bilioni 4,355,403,306.07
"Mheshimiwa Mkuu wa Wilaya lengo letu ilikuwa kukusanya zaidi ya bilioni tano lakini kwa sasa tumekusnya zaidi na kupata ziada shilingi 987,261,575.13 ambapo ni sawa na asilimia 122.7""alisema Akyoo.
Kwa Upande wa Tanesco Meneja wa Shirika hilo Uswege Abel Mwasaguti amsema vijiji vyote 70 vya Wilaya hiyo vina umeme na mitaa nane ambapo Wilaya ina vitongoji 393 hivyo katika Wilaya hiyo vitongoji 260 vina umeme na vitongoji 133 havina Umeme lakini kwa sasa vitongoji 65 vinashughulikiwa na wakandarasi wako kazini.
Kikao kazi hicho kililenga kufanya tathmini ya utekelezaji wa majukumu ya Taasisi, Idara na Vitengo kwa mwaka wa fedha 2025/2026, Kujadili muelekeo na mpango wa Taasisi hizo kwa mwaka wa fedha 2026/2027 na miaka mitano ijayo pamoja na kusikiliza na kutatua changamoto za watumishi.
MWISHO.

No comments:
Post a Comment