Kituo cha Afya Kizimkazi kutoa huduma ya usafishaji figo - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Thursday, 13 August 2026

Kituo cha Afya Kizimkazi kutoa huduma ya usafishaji figo

 





Rais Samia Suluhu Hassan, amesema Kituo cha Afya Kizimkazi kitatoa huduma ya kusafisha damu (dialysis), ikiwa ni sehemu ya hatua za kusogeza huduma za afya karibu na wananchi.


Rais Samia amesema hayo leo Agosti 13, 2026, wakati wa akizungumza na wananchi wa Kizimkazi baada ya kufanya uzinduzi wa miradi mbalimbali ukiwamo wa Kituo cha Afya Kizimkazi, ambapo pia amekabidhi gari la wagonjwa kwa ajili ya kusaidia huduma za afya katika eneo hilo.


Amesema huduma hiyo kwa kawaida hupatikana katika hospitali kubwa, lakini kuwepo kwa huduma hiyo katika Kituo cha Afya Kizimkazi ni hatua kubwa ya maendeleo katika sekta ya afya.


“Dialysis kawaida inapatikana katika hospitali kubwa tu lakini kwenye hospitali yetu hapa huduma hiyo ipo, kwa hiyo maendeleo ni makubwa,” amesema Rais Samia.

No comments: