Ndejembi: Tunakamilisha mtandao mpya, umeme wa JNHPP uwafikie Watanzania wote - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 22 August 2026

Ndejembi: Tunakamilisha mtandao mpya, umeme wa JNHPP uwafikie Watanzania wote

 



Waziri wa Nishati, Deogratius Ndejembi, amesema Serikali inatambua kuwa kuongeza uzalishaji wa umeme pekee haitoshi, hivyo inaendelea kuwekeza katika mtandao wa kusafirisha na kusambaza nishati hiyo ili kuwafikia wananchi wote.


Akizungumza katika uzinduzi wa Bwawa la Umeme la Julius Nyerere (JNHPP) leo Agosti 22, 2026, Ndejembi amesema mradi wa njia ya umeme ya TAZA wenye kilomita 617 na msongo wa KV 400 umefikia asilimia 98 ya utekelezaji.


Amesema njia hiyo inayopita Iringa, Mbeya na Songwe tayari inaunganisha Mkoa wa Rukwa kwenye Gridi ya Taifa, hatua inayotarajiwa kuimarisha upatikanaji wa umeme wa uhakika katika maeneo hayo.


“Si njia ya Taza pekee, kuna njia nyingine inatoka Songea- Tunduru- Masasi- Maumbika, itakayopeleka umeme wa uhakika mikoa ya Lindi na Mtwara ambako kumekuwa na changamoto ya upatikanaji wa nishati hiyo,”


 “Hivi tunavyoonngea mheshimiwa Rais mkandarasi yupo Tunduru anafanya kazi kuelekea Masasi. Kuongeza uwezo wa uzalishaji pekee hautoshi, lazima tuwe na mtandao wenye uwezo kupokea na kusafirisha umeme wote kwenye maeneo mbalimbali ya nchi,” amesema Ndejembi.


Aidha, amesema Serikali inaendelea kuwekeza katika Kituo cha Ibadakuli na kuandaa njia ya Tanzania-Uganda, huku ikiimarisha miundombinu ya usambazaji ili kupunguza changamoto ya kukatika kwa umeme kwa watumiaji.

No comments: