Rais Samia Suluhu Hassan, leo Jumamosi Agosti 22, 2026, amezindua rasmi Kituo cha Kuzalisha Umeme cha Julius Nyerere (JNHPP), kilichopo Rufiji, Mkoa wa Pwani.
JNHPP ni mradi mkubwa wa kimkakati katika sekta ya nishati nchini, wenye uwezo wa kuzalisha Megawati 2,115 kupitia mitambo tisa, kila mmoja ukiwa na uwezo wa Megawati 235.
Mradi huo umegharimu takribani Sh. trilioni 7.452, fedha za ndani za serikali na ujenzi wake ulianza Juni 2019 na kukamilika Machi 2025.


No comments:
Post a Comment