TFS YATAKIWA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA UHIFADHI KWA WANANCHI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 4 August 2026

TFS YATAKIWA KUENDELEA KUTOA ELIMU YA UHIFADHI KWA WANANCHI

 




Lilian Kasenene, Morogoro


maipacarusha20@gmail.com 


WAKALA wa Huduma za Misitu Tanzania (TFS) imetakiwa kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi wa mazingira ili kupunguza ukataji holela wa miti na vitendo vinavyoharibu vyanzo vya maji.


Mkuu wa Mkoa wa Morogoro Adam  Malima alisema hayo kwenye Maonesho ya  Nanenane 2026 Kanda ya Mashariki yanayofanyika mkoani Morogoro, ambapo alisisitiza umuhimu wa ushirikiano kati ya TFS na halmashauri katika kurejesha uoto wa asili na kuhifadhi mazingira.


Alisema wananchi wanapaswa kuhamasishwa kupanda miti kwa wingi, ikiwemo miti ya matunda na mazao ya viungo kama karafuu, ambayo pamoja na kuongeza kipato huchangia kuhifadhi mazingira na kulinda vyanzo vya maji.


"Ushirikiano kati ya TFS, halmashauri na wadau wengine wa mazingira ni muhimu katika kuhakikisha uoto wa asili unarejea na rasilimali za misitu zinaendelea kuhifadhiwa kwa manufaa ya vizazi vya sasa na vijavyo," alisema Mkuu wa Mkoa.


Kamanda wa TFS Kanda ya Mashariki, Mathew Ntilicha, alisema TFS inaendelea kutekeleza majukumu yake ya kulinda na kuhifadhi misitu ya hifadhi, kudhibiti uvunaji haramu wa mazao ya misitu, kuhamasisha upandaji miti, kurejesha maeneo yaliyoharibiwa, kutoa elimu kwa wananchi kuhusu uhifadhi wa mazingira na kusimamia matumizi endelevu ya rasilimali za misitu.


Ntilicha alisema taasisi hiyo itaendelea kushirikiana na halmashauri pamoja na wadau mbalimbali katika kutekeleza mkakati wa kurejesha uoto wa asili na kuhakikisha rasilimali za misitu zinalindwa na kutunzwa kwa manufaa ya Taifa.


Mwisho..

No comments: