NA SEIF TAKAZA, IRAMBA
maipacarusha20@gmail.com
HOSPITALI
ya Kiomboi Wilayani Iramba Mkoa wa Singida imepokea maiti 12 na Majeruhi wawili
waliopata ajali katika Mlima wa Sekenke leo asubuhi baada ya lori lililokuwa limebeba
mafuta kugonga gari dogo la Polisi
lilokua likotokea Shelui.
Kwa mujibu wa taarifa za awali, kutoka kwa Mganga Mkuu wa Wilaya ya Iramba Dkt Peter Luhega Janga amesema kuwa gari la Polisi lilikuwa likitoka Shelui
kuelekea Kiomboi, likiwa limewabeba askari watano (5) pamoja na mahabusu ambapo
Askari wote watano pamoja na mahabusu wamepoteza maisha katika
ajali hiyo.
Dereva wa lori na tingo wake wanadaiwa kuokolewa
na wananchi, huku taarifa za awali zikieleza kuwa wamejeruhiwa.
Akizungumza na Waandishi wa Habairi Dkt Janga amesema mapema asubuhi wapokea majeruhi wawili na marehemu 12 wakiwemo wanawake wawili na wanaume kumi .
" Mpaka sasa majeruhi wawili
wanaendelea vizuri akiwemo dereva wa lori la mafuta ambaye ni mwanchi wa Ruanda
" aleleza Dkt Janga
Hata hivyo Dkt Janga ameeleza kuwa
wananchi wa maeneo walikotoka Mahabusu hao wanaendelea na Zoezi la kuwatambua
huku askari mtaafu wa Jeshi la Wananchi Kapteni Onesmo Mbutu amemtambua kijana
wake Hassan Onesmo Mbutu (26) ambaye ametoka katika kijiji Cha Doromoni Kata ya
Tulya.
Wengine waliotambuliwa ni Vivian Saidi (60)mkazi i wa Kijiji cha Meli kata ya Old Kiomboi pamoa na Timoth Lazaro Kimaro wa Doromoni.
Mzazi wa Hassan Kapteni Onesmo Mbutu amesema mtoto wake alichukuliwa na Polisi kupelekwa Mahakamani Kiomboi kwa tuhuma ya kumdhamini rafiki yake aliyemdhamini katika mkopo wa ashilingi laki moja na nusu.
" Mimi nashangaa kuhusu kijana wangu ambaye inasemekana alimkopea rafiki yake fedha na alikua anaenda kuelewana na mhusika lili amlipe lakini alishtukia yuko mikononi mwa Polisi na kuelezwa anapellekwa Mahakamani Kiomboi"" alieleza kwa masikitiko makubwa huku machozi yakimlengalenga
MWISHO

No comments:
Post a Comment