DC IRAMBA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WATOA POLE KWA WAFIWA AJALI YA POLISI NA MAHABUSU - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 23 September 2026

DC IRAMBA NA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA WATOA POLE KWA WAFIWA AJALI YA POLISI NA MAHABUSU



Seif Takaza, Iramba


maipacarusha20@gmail.com


MKUU wa Wilaya ya Iramba Mkoa wa Singida Alhaj Suleiman Yusuf Mwenda na Kamati ya Usalama ya Wilaya hiyo ameenda kutoa pole kwa waliofiwa na kijana wao Timoth Kimaro aliepata ajali ya gari ya Polisi kugongwa na lori la mafuta lililokua likitokea Tanga.

Alhaj Mwenda pia alitoa salamu za pole kutoka kwa Waziri Mkuu Dkt Mwigulu Lameck Nchemba ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi.

Aidha Mkuu huyo Wilaya amesema amepokea Salamu za pole kutoka kwa Mkuu wa Polisi nchini IGP Camilius Wambura.

" Ndugu zangu kwa niaba ya Serikali ya Jamhuri ya Tanzania nawapeni pole kwa moyo wa dhati kabisa kwa vifo vya watu 12 akiwemo kijana wenu Timoth Kimaro na wengine hii ni kazi ya Mungu hivyo sisi sote tuwaombee kwa Mungu azilaze roho za Marehemu peponi lakini pia Mbunge wetu Dkt Mwigulu Nchemba anatoa pole amesema yuko pamoja nanyi katika kuomboleza misiba pole kwa niaba ya Wananchi wa Old Kiomboi ameishukuru Serikali kuanzia Waziri Mkuu, Mkuu wa Wilaya na IGP kwa kuwafariji wafiwa kwani ajali hiyo imepokelewa kwa masikitiko makubwa.


Naye Diwani Mstaafu wa kata ya Ntwike Albert Makwala kwa niaba ya wafiwa amesema pamoja na shukrani kwa Serikali ameomba yawepo mazungumzo kati ya ndugu na Serikali ili wajue kilicho msibu kijana wao marehemu Timoth Kimaro.

MWISHO

No comments: