Rick Ross amtaja Rais Samia mziki wa Tanzania kufika duniani - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Wednesday, 23 September 2026

Rick Ross amtaja Rais Samia mziki wa Tanzania kufika duniani

 



Mwandishi Wetu Maipac 


maipacarusha20@gmail.com 


Msanii wa miondoko ya Hip Hop kutoka Marekani, Rick Ross, amempongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Samia Suluhu Hassan, kwa kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia kwa kuibua vipaji vya wasanii na kupewa nafasi. 


Rick Ross amesema Tanzania imekuwa akilini mwake kwasababu ya kuwapo kwa vipaji vya muziki nchini.


“Heshima kubwa kwa Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia.” amesema katika ujumbe wake.


Msanii huyo pia ametaja uzuri wa Tanzania, akivitaja vivutio vya Serengeti na Zanzibar.


Ameeleza kuwa yuko tayari kuja kuitembea nchini hiyo na kutumia muda kukutana na Watanzania, kufahamu tamaduni na kupata uzoefu wa moja kwa moja.


Aidha, Rick Ross amesema yeye na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Paul Makonda, wana mipango mikubwa ya kushirikiana na tasnia ya muziki Tanzania, ikiwamo kufanya kazi na baadhi ya wasanii wakubwa nchini pamoja na kuwafikia wasanii wa kizazi kipya. 


“Kuna vipaji vya ajabu sana huko, na ninataka dunia ivione.” amesema, akisisitiza kuwa ushirikiano huo ndiyo kwanza unaanza.

No comments: