![]() |
| mbunifu wa bidhaa za lishe, Anne Christopher Kivuyo |
Mwandishi wetu, Arusha
maipacarusha20@gmail.com
Wabunifu wa bidhaa za lishe nchini wameiomba Serikali kuweza kuwawezesha kupata mitaji zaidi ili waendelee kubuni bidhaa zenye kiwango kikubwa Cha ubora.
Akiongea kwa niaba ya wabunifu bidhaa za lishe hapa nchini Bi Anne Christopher Kivuyo, ameomba Serikali kuwawezesha kupata mtaji mkubwa zaidi ili waweze kuongeza uzalishaji wa bidhaa zako kutoa ajira na kuzifikisha bidhaa hizo kwa wananchi katika maeneo mbalimbali.
Kivuyo amesema kuwa kwa upande wake yeye anachofanya kinahitaji kuwezeshwa zaidi kupitia upatikanaji wa masoko na eneo maalumu ambalo litawawezesha wateja kumfikia kwa urahisi, akieleza kuwa kwa sasa baadhi ya wateja hutumia namba zake za simu kumtafuta ili kupata bidhaa hizo.
" lengo Kubwa si kupata fedha pekee, bali kujenga chapa itakayoweza kuwasaidia wananchi kwa upana zaidi, huku akiamini kuwa mafanikio ya kifedha yatafuata baada ya bidhaa zake kuwafikia watu wengi"aliongeza
Pia alisema kuwa kwa sasa changamoto kubwa zinazomkabili ni gharama za vifungashio na utengenezaji wa lebo zenye viwango vinavyokidhi mahitaji ya bidhaa.
Amesema bidhaa inapokuwa katika kiwango kizuri, inahitaji pia kifungashio na lebo vinavyolingana na ubora huo.
Amesema ubunifu wa bidhaa ni mchakato unaohitaji muda na maarifa, hivyo amekuwa akiwafundisha watoto wake watatu kuhusu shughuli anazofanya ili kuhakikisha maarifa hayo yanaendelea hata pale ambapo yeye hatakuwa na nguvu za kuendelea na uzalishaji.
Amesema kwa mujibu wa uzoefu wake na maelezo anayoyatoa kuhusu bidhaa zake anaamini ina virutubisho vinavyoweza kuwa na manufaa kwa afya, ikiwemo kwa watoto.
Hata hivyo, Kivuyo ameeleza kuwa bado anakabiliwa na changamoto ya kuongeza uwezo wa uzalishaji kutokana na mahitaji ya bidhaa zake kuongezeka. Amesema baadhi ya wateja kutoka nje ya mkoa wamekuwa wakihitaji bidhaa hizo, lakini uwezo wake wa sasa haujatosheleza mahitaji yote.
Kwa msingi huo, Kivuyo ameiomba Serikali na wadau wengine wa maendeleo kumsaidia kupata mtaji, masoko na mazingira mazuri ya kukuza biashara yake ili aweze kuongeza uzalishaji, kutoa ajira na kusafirisha bidhaa zake kwenda maeneo mbalimbali nchini.

No comments:
Post a Comment