
MWENYEKITI WA TAASISI YA MAENDELEO YA KIISLAAM (IDF)SHEIKH OMARI MUNA AKIFUNGA KIKAO CHA VIONGOZI WA IDF MKOA WA SINGIDA KASKAZINI KILICHOFANYIKA UKUMBI WA RAFIKI RESORT MJNI SINGIDA
NA SEIF TAKAZA SINGIDA
maipacarusha20@gmail.com
MWENYEKITI wa Taasisi ya Maendeleo ya Kiislaam IDF
Mkoa wa Singida Kaskazini Shekh
Omar Muna amewataka Waislaam kuhakikisha watoto wao wanapata Elimu ya Dini wakiwa shuleni ili wawe na
hofu ya Mungu wakiwa wadogo
Agizo hilo limetolewa jana wakati
wa kikao cha siku moja kilichohusu
Maendeleo ya Kiislaam hususn Elimu ya Dini kwa watoto wa Shule za Msingi na
Sekondari yaliyofanyika kaka Ukumbi wa Rafiki Resort sabasaba
mjini Singida
Amesema ni jukumu la kila kiongozi
wa Kiislaam bila kujali madhehebu ya dini
ya Kiislaam yaliyopo kuhakikisha
Uislaam unasonga mbele katika nyanja zote.
Amesema kuwa
Taassisi ya IDF inayo malengo ya kuendeleza Uislaam kwa nyaja zote ili W aislaa wapate Maendeleo
ya Dini na ya Kiuchumi.
Naye Mwenyekiti wa IDF kanda ya
kati katika kutoa maelezo kuhusu malengo na madhumuni ya Taasisi hiyo kwa
wajumbe wa IDF Mkoa wa
Singida Kaskazini amesema lengo la
Taasisi hiyo
Kwa upande wake Mwenyekiti wa
Kanda ya kati Mrisho Pesambili alieleza kuwa Taasisi hiyo ina idara saba
ambazo zitahusika moja kwa moja malengo yaliyokusudiwa ambapo viongo,I wa
Kitaifa wametoa maelekezo ya maana ya dhima ya Taasisi hiyo yenye
dhamira ya kushiriki katika kuimarisha Misingi ya Dini ya Kiislaam na kuchangia
Maendeleo ya kijamii.
Kuwa kila eneo katika Idara
saba una gsAidha alisisitiza kuwa IDF
ina lengo la kujenga jamii yenye uelewa
wa Dini kwa kufuata maadili mama, Elimu
na uwezo kujitegemea kiuchumi
Naye Katibu wa Kanda ya Kati
Abdulqadir Shangali ameeleza kika hicho
kuwa muundo wa Taasisi hiyo unalenga kuweka mgawanyo wa majukumu na kuhakikisha una shughuli
na uangalizi unaostahili.
Wajumbe wa kikao hicho kwa kauli
moja walikubaliana kuipokea IDF na watajitahidi
kufanya kazi kwa pamoja kuhakikisha Taasisi hiyo inafikia malengo yaliyokusudiwa.
MWISHO
No comments:
Post a Comment