Shule ya Santa Edwin Yapongezwa kwa Mazingira Bora ya kitaaluma na maadili. - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Saturday, 26 September 2026

Shule ya Santa Edwin Yapongezwa kwa Mazingira Bora ya kitaaluma na maadili.

 




Mgeni Barkat Firoz Khan akitoa hotuba yake kwenye mahafali ya tatu ya Santa Edwin Pre and Primary

Mkurugenzi Msaidizi wa Santa Edwin Pre and Primary Lulu Samson Soko alieleza maono ya Mkurunzi kwenye kuifanya Shule hiyo kuwa miongoni mwa Shule bora

Hassan Ibrahimu, Mwalimu Mkuu wa Santa Edwin akieleza mikakati ya Shule mbele ya Mgeni Rasmi


 Mwandishi wetu, MWANZA


Shule ya Santa Edwin Pre and Primary School ya Majengo Mapya, Nyegezi jijini Mwanza, imefanya mahafali yake ya tatu, ikiwa ni sehemu ya kuhitimisha hatua muhimu ya masomo kwa wanafunzi pamoja na kutambua mchango wa walimu, wazazi na uongozi wa shule.


Mahafali hayo yaliyofanyika Septemba 24, 2026, yalihudhuriwa na wageni mbalimbali, huku Barkat Firoz Khan, Afisa Rasilimali Watu kutoka Furaha Company Ltd ya jijini Mwanza, akiwa Mgeni Rasmi.


Akizungumza katika hafla hiyo, Khan aliipongeza Santa Edwin kwa juhudi inazofanya katika kuboresha kiwango cha elimu na matokeo ya wanafunzi katika mitihani mbalimbali, ikiwemo mitihani ya kitaifa.


Alisema mafanikio ya shule hayawezi kutenganishwa na ushirikiano wa karibu kati ya walimu, wazazi na wanafunzi, akisisitiza umuhimu wa kujenga mazingira yanayochanganya ufaulu wa kitaaluma na malezi yenye maadili.


“Nashauri walimu, watoto na wazazi kuendelea kufanya kazi kwa pamoja ili kuhakikisha shule inatoa watoto wenye ufaulu mzuri na maadili mema,” alisema Khan.


Kwa upande wake, Mkurugenzi Msaidizi wa Santa Edwin Lulu Samsoni Soko  alisema uongozi wa shule utaendelea kuweka msisitizo katika utoaji wa elimu bora na malezi yanayomjenga mwanafunzi kitaaluma, kitabia na kijamii.

Wahittimu

Naye Mwalimu Mkuu wa Santa Edwin, Hassan Ibrahimu, alisema mafanikio yaliyopatikana hadi sasa yametokana na mshikamano na ushirikiano kati ya uongozi, walimu na wazazi.


Alisema shule itaendelea kuimarisha ushirikiano huo ili kuhakikisha wanafunzi wanapata mazingira bora ya kujifunza na kukuza vipaji vyao.


Katika mahafali hayo, wanafunzi waliofanya vizuri katika masomo mbalimbali na walioonesha umahiri katika maeneo tofauti walitunukiwa zawadi. Aidha, baadhi ya wafanyakazi wa shule walipewa zawadi kama kutambua mchango wao katika maendeleo ya shule.


Mahafali hayo yamekuwa pia fursa kwa shule, wazazi na wadau wa elimu kutafakari mafanikio yaliyopatikana na kuweka msisitizo katika kuendelea kuboresha elimu, malezi, vipaji na maadili ya watoto.

No comments: