Na Lilian Kasenene, Morogoro
Maipacarusha20@gmail.com
DEREVA kutoka nchini Kenya Karan Patel, ameendeleza ubabe wake katika mashindano ya mbio za magari baada ya kuibuka mshindi wa kwanza na kutwaa ubingwa wa Afrika kupitia mashindano ya Serengeti Rally of Tanzania 2026 yaliyofanyika mkoani Morogoro.
Patel, akiwa pamoja na mwongozaji wake Tauseef Khan, wameonyesha kiwango bora katika mashindano hayo na kuonesha uwezo mkubwa katika kipindi chote cha mbio.
Mashindano hayo yamefanyika kwa siku nne, kuanzia Oktoba 1 hadi 4, 2026, katika Msitu wa TFS mkoani Morogoro, yakihusisha washindani kutoka mataifa mbalimbali, yakiwemo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, Zambia na Tanzania, ambayo ilikuwa mwenyeji wa mashindano hayo.
Katika matokeo ya jumla, nafasi ya kwanza ilichukuliwa na Karan Patel na mwongozaji wake Tauseef Khan kutoka timu ya Asas, huku nafasi ya pili ikichukuliwa na dereva Manveer Bird wa Tanzania, akiwa na mwongozaji wake Zubayr Piredina, ambao pia wanaiwakilisha timu ya Asas.
Mashindano hayo yamekuwa na ushindani mkubwa, yakileta pamoja madereva na waongozaji kutoka mataifa mbalimbali, huku Tanzania ikipata nafasi ya kuwa mwenyeji wa moja ya mashindano makubwa ya magari barani Afrika.
...........


No comments:
Post a Comment