Makatibu wa Mabunge watembelea hifadhi ya Ngorongoro - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 6 October 2026

Makatibu wa Mabunge watembelea hifadhi ya Ngorongoro

 



Makatibu wa Mabunge kutoka mataifa mbalimbali duniani wanaoshiriki Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU 153), leo Oktoba 6, 2026, wametembelea Hifadhi ya Ngorongoro, Arusha, kujionea kwa karibu utajiri wa urithi, utamaduni na maajabu ya asili yanayopatikana katika eneo hilo.


Ziara hiyo imeanzia katika Makumbusho ya Urithi Geopark, ambako wajumbe hao wamepata fursa ya kujifunza kuhusu historia ya kijiolojia, akiolojia, utamaduni na urithi wa eneo la Ngorongoro.


Baada ya hapo, wameendelea na ziara katika Kasoko ya Ngorongoro (Ngorongoro Crater), ambapo wamejionea mandhari ya kuvutia pamoja na aina mbalimbali za wanyamapori, wakiwemo wanyama wakubwa watano maarufu “Big Five.”


#IPUTanzania153

No comments: