MARTHA MLATA AMNADI KINOTA JB DIWANI KATA YA SHELUI - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Monday, 19 October 2026

MARTHA MLATA AMNADI KINOTA JB DIWANI KATA YA SHELUI

 

 

MGOMBEA UDIWANI WA KATA YA SHELUI  CCM OMARI HAMISI KINOTA JB AKIPIGA MAGOTI KUOMBA RIDHA KWA WANANCHI WAMPIGIE KURA KATIKA UCHAGUZI MDOGO KATA YA SHELUI


 SEIF  TAKAZA IRAMBA 


maipacarusha20@gmail.com 


MWENYEKITI wa Chama cha Mapinduzi Mkoa Singida  Marther Mlata amezindua rasmi kampeni ya Uchaguzi mdogo wa Udiwani  kata ya Shelui iliofanyika juzi  Mkwajuni mji mdogo wa Shelui baada ya Diwani wa kata hiyo kufariki dunia .

 

 

Mlata akimnadi Mgombea  wa  kata hiyo Omari Hamisi Kinota jina maarufu JB  akimumuelezea kuwa ni mtu makini  mtu wa watu,mwadilifu  mwenye uwezo kutumikia jamii  kushirikian na jamii katika changamoto mbalimbali lakini ana uwezo wa kujenga hoja si mwepesi wa  kukata tamaa

 

 

"Ndugu zangu wanachama wa CCM na wananchi wote kwa ujumla mimi ninvyomfahamu Kinota akiwa mjumbe wa Hallmashauri Kuu ya Mkoa lakini pia mjumbe wa Mkutano Mkuu wa Taifa akitaka kutetea jambo la Maendeleo ni mzuri katika kujenga hoja na ni mwepesi wa kufuatilia kwa hiyo ndugu zangu nawaomba siku ya Uchaguzi tarehe nne mwezi  ujao  Chagueni Chama Cha Mapinduzi na mchagueni Kinota " alisisitiza Mlata huku akishangiliwa na wananchi

 

 

Mwenyekiti huyo ambaye amepambwa na sifa ya uongozi bora kwa kila aliyesimama kumnadi mgombea  huku wanachama wa  CCM wakimshangilia kwa dalili ya kumuunga mkono Kinota alisema kwa sasa hivi  waache makundi wawe kitu kimoja ili Kinota awe Diwani wa Kata ya Shelui.

 

Aidha Mlata ameowaomba wagombea walioshindania katika kinyang'anyro cha  nafasi hiyo wamuunge mkono ili Chama cha Mapinduzi kiweze kushinda . 

Hata hivyo aliwasimamisha wagombea wawli kati ya wagombea sita waliogombea na Kinoata na kuahidi  kuwa pamoja katika kampeni na kuhakikisha Kinota anashinda uchaguzi huu.

 

Naye Mgombea wa Udiwani wa kata hiyo Omari Hamisi Kinota amewaomba wananchi wa kata hiyo huku akiwa amepiga magoti kwa heshima amesema anaomba wananchi wampe kura za ndiyo. na kuahidi kuwasaidi wananchi wake kwa hali na mali.

 

 

"Ndugu zangu nawaomba kwa ridhaa yenu siku ya tarehe nne mwezi ujao mnipe kura zenu zote  ili niweze kuwatumikia kama kipindi  nilipokua diwani wa kata hii,   jamani mimi ni binaadamu kama niliteleza kipindi kile nimekuja kwenu tena naomba wale wote tuliokuwa tukipambana katika kura za maoni naomba tusameheane ili mnipe fursa nyingine niweze kuwatumikia." Alisema JB huku akipigiwa makofi

 

Kwa upande wake mwananchi mmoja ambae hakutaka jina lake litajwe kwenye vyombo vya habari alisema kuwa Kinota anamfahamu  anao uzoefu mkubwa  wa kuwatumikia wananchi na akijenga hoja  yake huwa  inakubalika hivyo

 

kijana huyu ana kipaji cha pekee tusimuangushe ,JB akikazania jambo anahakikisha linatimia.

 

 

"Ndugu yangu Mwandishi wa habari mimi ni mwenyeji wa kata hii hasa hapa Shelui JB anao uwezo wa kupambana ili asaidie jamii  ni mfano mmoja wa  Kituo cha Afya wakati ule akiwa Diwani alifanya chini juu hadi sasa tunatumia  tunamuombea dua  kwa Mwenyeezi Mungu amjaalie eweze kushinda,  kitu kingine kuhusu maji kutoka Ziwa Victoria alipambania hadi sasa Shelui haina shida ya Maji" alisema 


====

No comments: