Spika wa Seneti Kenya atembelea Banda la Tanzania Mkutano wa IPU 153 Spika wa - MAIPAC MEDIA TANZANIA

Breaking

MAIPAC MEDIA TANZANIA

A Centre for Indigenous and Pastoralists Community Informations




Tuesday, 6 October 2026

Spika wa Seneti Kenya atembelea Banda la Tanzania Mkutano wa IPU 153 Spika wa

 


Spika wa Bunge la Seneti la Kenya, Amason J. Kingi, EGH, akipokea maelezo kuhusu safari ya Tanzania katika demokrasia na mchango wake katika kukuza amani na usalama barani Afrika na duniani, alipotembelea Banda la “Karibu Tanzania” katika Mkutano wa 153 wa Umoja wa Mabunge Duniani (IPU), unaofanyika jijini Arusha.


Akiwa katika Banda hilo, Kingi alipata fursa ya kufahamu hatua mbalimbali zilizopigwa na Tanzania katika maendeleo, hususan katika sekta za miundombinu, afya, elimu na usawa wa kijinsia, pamoja na utekelezaji wa Ajenda ya 2030 ya Malengo ya Maendeleo Endelevu (SDGs) na mwelekeo wa kimkakati wa utekelezaji wa Dira ya Taifa ya Maendeleo 2050.


#IPU153Tanzania

No comments: